Maelezo mafupi ya Maumivu ya Kichwa

Imepitiwa/Imerekebishwa Mar 2023

Maumivu ya kichwa ni mojawapo ya sababu za kawaida za watu kwenda kwa daktari.

Je, maumivu ya kichwa husababishwa na nini?

Vyanzo vya kawaida vya maumivu ya kichwa ni:

Vyanzo vingine vya maumivu ya kichwa ni:

Je, ninapaswa kuona daktari kwa maumivu ya kichwa wakati gani?

Muone daktari mara moja ikiwa unaumwa na kichwa na una mojawapo ya dalili zifuatazo za tahadhari:

  • Mabadiliko katika kuona kwako, udhaifu, kusinzia, kuchanganyikiwa, kutoweza kuwa wima, au kutatizika kuzungumza

  • Homa na shingo kukaza

  • Maumivu makali ya kichwa yanayotokea ghafla kama ngurumo

  • Maumivu pande za kichwa (kama unapochana nywele) au maumivu ya taya unapotafuna

  • Saratani, UKIMWI, au mfumo dhaifu wa kingamwili

  • Kuongezeka kwa maumivu ya kichwa

  • Macho kuwa mekundu na kuona vimulimuli ukiwa karibu na taa

Muone daktari ndani ya wiki moja ikiwa una:

  • Maumivu ya kichwa ambayo huanza baada ya kufikia miaka 50

  • Kupoteza wezo wa kuona

  • Kupungua uzani

  • Maumivu ya kichwa ambayo yanazidi kuongezeka au ya mara kwa mara

Ikiwa una umri wa zaidi ya miaka 50, maumivu yoyote mapya ya kichwa au mabadiliko ya maumivu ya zamani ya kichwa yanapaswa kuchunguzwa na daktari. Watu wazee wana uwezekano mkubwa wa kuwa na vyanzo vikubwa vya maumivu ya kichwa, na hata maumivu ya kichwa ya kawaida yanaweza kuwa vigumu zaidi kutibu kwa wazee.

Je, nitarajie nini ninapokwenda kumwona daktari wangu?

Daktari wako atakuuliza maswali kuhusu dalili zako na kukuchunguza. Daktari wako anaweza pia kufanya vipimo kama vile:

Je, madaktari hutibu vipi maumivu ya kichwa?

Matibabu yanategemea aina ya maumivu ya kichwa uliyo nayo:

  • Ikiwa tatizo lingine la kiafya linasababisha maumivu ya kichwa, madaktari watalitibu tatizo hilo

  • Kwa maumivu ya kichwa yanayotokana na shinikizo au maumivu ya kichwa yanayotokana na virusi, madaktari watakuagiza unywe dawa za maumivu kama vile aspirini, asetaminofeni, au ibuprofeni.

  • Kwa kipandauso, madaktari watakupa dawa maalum