Maumivu ya Kichwa Yanayotokea kwa Awamu

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2024

Je, maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu ni nini?

Maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu ni aina fulani ya maumivu ya kichwa. Maumivu haya ya kichwa hutokea kwa awamu, hii inamaanisha kuwa unapata kiasi kikubwa cha maumivu ya kichwa kwa muda kisha yanapotea.

  • Maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu ni ya kawaida zaidi kwa wanaume kuliko wanawake

  • Una maumivu makali nyuma ya jicho moja au upande mmoja wa kichwa chako

  • Kwa upande huo wa maumivu ya kichwa, pua lako linaziba na jicho lako linakuwa na machozi

  • Maumivu ya kichwa kwa kawaida huchukua chini ya saa moja lakini hurudi angalau mara moja kwa siku kwa mwezi au zaidi

  • Unaweza kuwa na kipindi kirefu bila kuwa na maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu

  • Matibabu ni pamoja na kupewa oksijeni kupitia maski ya uso na dawa

  • Unawezahitaji kumeza dawa ili kuzuia mashambulizi

Je, ni nini husababisha maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu?

Madaktari hawana uhakika kuhusu kinachosababisha maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu. Hata hivyo, pombe inaweza kuchochea maumivu ya kichwa wakati wa kipindi cha awamu.

Je, dalili za maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu ni zipi?

Maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu huanza ghafla. Dalili ziko upande mmoja wa kichwa chako na ziko upande huo kila wakati. Katika shambulizi:

  • Utakuwa na maumivu makali sana katika sehemu ya jicho moja na upande huo huo wa kichwa chako

  • Maumivu huongezeka ndani ya dakika chache na kwa kawaida huchukua nusu saa hadi saa

  • Maumivu yanaweza kukuamsha kutoka usingizini na ni makali sana kiasi cha kukufanya uhisi kutaka kutembea huku na kule

  • Unaweza pia kuwa na pua iliyoziba, inayotiririka na jicho la majimaji kwa upande sawa na maumivu

Mashambulizi hutokea mara moja au zaidi kwa siku, mara nyingi kwa wakati mmoja wa mchana au usiku. Kwa kawaida hutokea mara kwa mara kwa muda wa mwezi 1 hadi miezi 3 (kinachoitwa kipindi cha awamu ya maumivu ya kichwa). Kisha miezi au miaka inaweza kupita kabla ya mashambulizi kutokea tena.

Ingawa dalili ni kali na hazipendezi sana, maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu sio hatari na hayaleti uharibifu wa ubongo.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu?

Madaktari wanashuku kuwa una maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu kutokana na dalili zako. Ili kuhakikisha kuwa maumivu yako ya kichwa hayasababishwi na kitu kingine, wanaweza kufanya:

Je, madaktari hutibu vipi maumivu ya kichwa yanayotokea kwa awamu?

Ili kutibu maumivu ya kichwa mara tu yanapoanza, madaktari wanaweza kukupa:

  • Oksijeni kupitia maski ya uso

  • Dawa zinazoitwa triptani kwa njia ya sindano au dawa ya kupulizia puani

Triptan pia hutumika kutibu kipandauso.

Ili kuzuia kupata maumivu zaidi ya kichwa, huenda ukahitaji:

  • Tembe za Kotikosteroidi

  • Kizuizi cha neva (kudungwa sindano ya dawa ya kufisha ganzi kwenye neva nyuma ya kichwa chako)

  • Dawa kama zile zinazotumika kuzuia kipandauso

  • Lithiamu