Nyenzo za Mada
Glaukoma ni nini?
Glaukoma ni ugonjwa wa macho ambao husababisha kupoteza uwezo wa kuona. Kwa kawaida hufanyika wakati shinikizo kutoka kwenye kiowevu cha ziada ndani ya mboni ya macho kinaharibu neva kwenye jicho lako (neva ya optiki).
Kupoteza uwezo wa kuona kwa kawaida hufanyika polepole, kwa hivyo huenda usigundue mara moja
Glaukoma huzidi kuwa mbaya kadiri muda unavyoenda.
Inaweza kusababisha kupoteza uwezo wa kuona kunakodumu na upofu isipotibiwa
Vitone maalum kwenye macho (vilivyoelekezwa na daktari wako) vinaweza kususha shinikizo machoni mwako
Fanyiwa uchunguzi kamili wa macho kila mwaka 1 hadi 2 ili kutambua glaukoma mapema na kusaidia kuzuia kupoteza uwezo wa kuona
Ikiwa una glaukoma, daktari atahitaji kuangalia shinikizo machoni mwako mara nyingi
Ni nini husababisha glaukoma?
Glaukoma hutokea ikiwa kiowevu kinaunda kwa wingi kwenye jicho lako, ambalo huongeza shinikizo ndani ya jicho lako.
Jicho lenye afya limejaa kiowevu. Kiowevu hicho husaidia kudumisha umbo linalofaa. Majimaji mara zote hutengenezwa na kisha kutoka nje. Wakati ukifanya kazi vizuri, mfumo huo hufanya kazi kama mfereji na kitoa maji kwenye karo. Usawa kati ya uzalishaji wa majimaji na mtiririsho wa majimaji—kati ya mfereji uliofunguliwa na karo linalotiririsha maji vizuri—hufanya majimaji yaendelee kutiririka bila kuzuizi na huepusha shinikizo kutokea kwenye jicho.
Katika glaukoma, majimaji hujikusanya kwa sababu kitu huzuia njia ya kawaida ya mtiririsho wa majimaji.
Kwa watu wengi, kisababishaji cha kiowevu kujiunda hakijulikani
Kwa baadhi ya watu, mtiririsho wa majimaji unazuiwa na tatizo lingine la jicho, kama vile maambukizi au uvimbe
Unaweza kupata glaukoma katika umri wowote, lakini ni ya kawaida zaidi unapozeeka.
Watu walio na hatari kubwa zaidi ya kupata glaukoma wanaweza kuwa na:
Wanafamilia ambao wana (au walikuwa) ugonjwa
Matatizo ya kuona (ugumu kuona vitu vilivyo karibu au mbali sana)
Matumizi ya muda mrefu ya dawa zinaitwa kotikosteroidi
Jeraha au upasuaji wa jicho wa awali
Dalili za glaukoma ni zipi?
Kwa kawaida dalili hutokea polepole kwa miezi au miaka:
Sehemu za mboni isiyoona (viraka vya maeneo ambayo huwezi kuona) kwa moja au macho yote mawili
Sehemu za mboni isiyoona kwa kawaida kwenye pande kwanza, kisha katikati
Wakati mwingine wekundu wa macho au kuhisi vibaya machoni, uoni hafifu au kuumwa na kichwa
Kupoteza uwezo wa kuona hufanyika polepole sana ambavyo huenda usigundue hadi wakati uwezo wako mkubwa wa kuona kupotea.
Wakati mwingine dalili hutokea kwa ghafla. Uvamizi wa ghafla wa glaukoma unaweza kuwa dharura ya kimatibabu. Unaweza kuwa na:
Uchungu mkubwa zaidi kwa macho na kuumwa na kichwa
Wekundu wa macho wa ghafla, uoni hafifu na kupoteza uwezo wa kuona
Kuhisi ni kama unataka kutapika
Kuuna miviringo iliyo na rangi ya upinde wa mvua kando ya taa
Madaktari wanawezaje kujua kama nina glaukoma?
Madaktari watakufanyia uchunguzi kamili wa macho. Watapima shinikizo kwenye macho yako, kupima sehemu za mboni isiyoona na kuangalia ndani ya jicho lako ili kuangalia neva yako ya optiki kwa ishara za kuharibika.
Madaktari hutibu vipi glaukoma?
Daktari wako atakupatia dawa (kwa kawaida vitone kwenye macho) ili kupunguza shinikizo kwenye macho yako. Wakati mwingine daktari wako atapendekeza upasuaji.
Hauwezi kurejesha uwezo wa kuona uliokuwa umepoteza, lakini unaweza kuzuia upotezaji zaidi wa uwezo wa kuona ikiwa unadhibiti shinikizo kwenye macho yako. Utahitaji kutibu glaukoma yako kila siku kwa maisha yako yote, kwa kawaida hata kama ulifanyiwa upasuaji.
Shinikizo kwenye macho yako litahitaji kukaguliwa mara nyingi na daktari wa macho ili kuhakikisha kuwa linasalia katika kiwango kizuri. Ikiwa si hivyo, daktari wako anaweza kuhitaji kubadilisha aina ya dawa unayotumia.
Nina wezaje kuzuia kupoteza uwezo wa kuona kutokana na glaukoma?
Ikiwa uko kwa hatari ya glaukoma, fanyiwa uchunguzi kamili wa macho kila mwaka 1 hadi 2. Hivyo, ikiwa daktari wako atapata kuwa una glaukoma, unaweza kuanzia matibabu ili kupunguza shinikizo kwenye macho yako, hata kama hauna dalili bado. Matibabu ya kila siku yatahitajika ili kuzuia kupoteza uwezo wa kuona.