Sanasitisi

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Je, sanasitisi ni nini?

Sanasi zako ni nafasi tupu zilizo na uwazi nyuma ya mashavu na paji la uso wako. Kila sanasi hufungukia kwenye pua yako. Sanasitisi ni hali ya kuvimba au kupata maambukizi kwa sanasi yako moja au zaidi.

  • Virusi, bakteria, kuvu na mizio inaweza kusababisha sanatisi

  • Unaweza kuwa na pua zilizojaa, pua zinazotoa makamasi, na maumivu kwenye uso au kichwa chako

  • Sanasitisi ambayo inadumu kwa zaidi ya miezi 3 inaitwa sanasitisi sugu

  • Madaktari hukupatia dawa ya kusaidia sanasi zako kutoa majimaji, na pia wanaweza kukuandikia dawa za kuua bakteria

Kufikia Sanasi

Je, nini husababisha sanasitisi?

Kwa kawaida sanasitisi husababishwa na:

  • Maambukizi ya virusi kwenye njia ya juu ya hewa (kama vile mafua)

Maambukizi ya virusi husababisha tishu za ndani ya pua zako kuvimba. Hii ndio sababu pua yako hujaa pale unapopata mafua. Kuvimba ndani ya pua yako huziba uwazi wa sanasi zako, hivyo kufanya majimaji kujikusanya ndani ya sanasi. Mizio pia hufanya sehemu ya ndani ya pua zako kuvimba na inaweza kusababisha sanasitisi.

Wakati mwingine, bakteria huingia kwenye majimaji ya sanasi na kusababisha:

  • Sanasitisi ya bakteria

Sanasitisi sugu hutokea mara kwa mara kama una:

  • Mizio

  • Polipu za pua

  • Unakaa kwenye hewa chafu au moshi wa tumbaku

  • Wanafamilia ambao hupata sanasitisi mara kwa mara

Je, dalili za sanasitisi ni zipi?

Dalili zinajumuisha:

  • Usaha wa kijani au njano (majimaji mazito) kutoka kwenye pua zako

  • Shinikizo na maumivu kwenye uso wako

  • Pua kufungana

  • Harufu mbaya mdomoni

  • Kukohoa makohozi, hasa usiku

  • Wakati mwingine, kuwa mgonjwa mwili mzima, kupata homa, na mzizimo

Nenda kamuone daktari mara moja iwapo una dalili hizi na pia maumivu makali ya kichwa na kuchanganyikiwa kwa sababu maambukizi yanaweza kusambaa hadi kwenye ubongo wako (homa ya uti wa mgongo)

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina sanasitisi?

Madaktari anaweza kubainisha kulingana na dalili zako na kwa kufanya uchunguzi. Wakati mwingine, madaktari hufanya:

  • Uchanganuzi wa CT (tomografia ya kompyuta) ili kuona kama maambukizi yamesambaa au kama una sanasi sugu

  • Endoskopia (kuweka bomba jembamba lenye hadubini ndani ya pua ili kutazama sanasi)

Je, madaktari hutibu vipi sanasitisi?

Madaktari hutibu sanasitisi kwa kuzisaidia sanasi zako kutoa majimaji. Daktari atakuambia: 

  • Kuvuta mvuke kutoka kwenye maji ya moto ya kuoga

  • Kwa kuweka taulo mbichi, za moto kwenye uso wako (juu ya sanasi zako)

  • Kwa kunywa vinywaji vya moto

  • Kupitisha mchanganyiko chumvi na maji kwenye pua zako au kutumia kinyunyizio cha maji na chumvi

  • Kwa kutumia kinyunyizio cha kupunguza msongamano, kama vile fenilefrina

Ikiwa una homa, maumivu makali, au sanasitisi ambayo hudumu kwa zaidi ya siku 10, kwa kawaida madaktari watakuandikia dawa za kuua bakteria.

Ikiwa una sanasitisi sugu (sanasitisi ambayo huduma kwa zaidi ya siku 90) madaktari wanaweza:

  • Kukufanya utumie dawa za kuua bakteria kwa wiki 4 hadi 6

  • Kufanya upasuaji ili kuondoa sanasi zako na kuzikamua majimaji