Ugonjwa wa Kuchochewa kwa Fupanyonga (PID) ni nini?
PID ni maambukizi kwenye uterasi (mfuko wa uzazi), kwenye mirija ambayo inaunganisha ovari zako na uterasi yako (mirija ya uzazi), au zote mbili. PID pia inaweza kusambaa kwenye ovari zako (viungo vya ngono ambavyo vinashikilia mayai yako) na kwenye mtiririko wa damu.
Maambukizi unayopata wakati wa kushiriki ngono yanayoitwa STI (maambukizi ya zinaa) yanasababisha PID
Bakteria (vijidudu) kutoka kwenye uke wako (njia ya uzazi) zinaingia kwenye uterasi yako
Utakuwa na maumivu katika sehemu ya chini ya tumbo na kwa kawaida vitu kutoka ukeni (majimaji mazito kutoka kwenye uke wako)
PID inaweza kuifanya ngumu kupata mimba (ugumba)
PID kwa kawaida hutokea kwa wanawake walio amilifu kwa ngono na inaweza kuwa kali sana
Madaktari hutibu PID kwa kutumia dawa za kuua bakteria
Ni nini husababisha PID?
Dalili za PID ni zipi?
Dalili za mapema za PID
Maumivu katika sehemu ya chini ya tumbo, ambayo yanaweza kuwa mabaya zaidi katika upande mmoja kuliko mwingine
Kuvuja damu ukeni ambao si sehemu ya hedhi yako ya kila mwezi
Vitu kutoka ukeni, ambavyo vinaweza kutoa harufu mbaya
Dalili za baadaye za PID
Maumivu makali sana katika sehemu ya chini ya tumbo
Homa (kwa kawaida huwa chini ya 102° F [38.9° C] lakini inaweza kuongezeka zaidi)
Kuhisi mgonjwa kwenye tumbo lako au kutapika
Vitu kutoka ukeni ambavyo ni vya rangi ya manjano-kijani au vinavyokaa usaha
Uchungu wakati wa ngono au wakati wa kukojoa (kutoa mkojo)
Dalili ambazo hutokea kuelekea mwisho wa hedhi yako ya kila mwezi au katika siku chache baada ya hedhi yako kuisha zinaashiria uwepo wa PID. PID inaweza kuwa kali lakini isababishe dalili kiasi au kutokuwa na dalili.
PID inaweza kusababisha matatizo mengine?
Ndiyo. Maambukizi kwenye PID yanweza kuenea kando ya sehemu ya ndani ya tumbo yako na kando ya ini lako. Wakati mwingine mkusanyiko wa usaha (usaha) hujiunda kwenye mirija yako ya uzazi.
PID inaweza kusababisha tishu ya kovu kujiunda kwenye mirija yako ya uzazi. Tishu hii ya kovu inaweza kukuzuia kupata ujauzito. Ikiwa tishu ya kovu inajiunda ndani ya tumbo lako (minato), matumbo yako yanaweza kukamatwa kwenye tishu ya kovu na kuzungushwa kufungika (kuzuizi cha utumbo).
Pia, ikiwa umekuwa na PID na uwe mjamzito, kuna una uwezekano mkubwa zaidi wa kuwa na ujauzito wa nje ya kizazi. Kwa ujauzito wa nje ya kizazi, mtoto wako anakua nje ya uterasi yako. Mtoto wako akikua kwenye mojawapo ya mirija yako ya uzazi badala ya uterasi yako, baada ya wiki kadhaa, mtoto anayekua hufanya mrija ugawanyike na kuwa wazi. Mtoto atafariki na mrija unaweza kuvuja damu sana ambavyo unaweza kufariki
Daktari wangu atajua vipi kuwa nina PID?
Daktari atakuuliza maswali na kwa kawaida kufanya uchunguzi ya fupanyonga. Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, daktari wako huchunguza sehemu ya ndani ya uke wako kwa kuufungua akitumia kifaa kidogo kinachoitwa spekulumu. Daktari wako anaweza:
Kuchukua sampuli ya kiowevu kutoka kwenye mlango wako wa kizazi kwa kutumia kipande cha pamba ili kuipima kwa ajili ya kisonono na klamidia
Kuamuru kipimo cha damu
Daktari akifikiri kuwa unaweza kuwa na usaha au ujauzito kwenye mrija wa uzazi wako, kwa kawaida utafanyiwa kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti.
Daktari wangu atatibu aje PID?
Kwa sababu STI (kisonono na klamidia) ndio visababishaji vyenye uwezekano kubwa za PID, daktari wako atakuandikia dawa za kuua bakteria ili kutibu STI hizo. Kwa kawaida utadungwa sindano moja na kisha umeze dawa za kuua bakteria nyumbani kwa wiki kadhaa. Usipoanza kupata nafuu ndani ya saa 48, unaweza kuhitaji kwenda hospitalini. Unaweza kutibiwa hospitalini mara moja ikiwa:
Una dalili kali zaidi au homa kali
Una usaha kwenye mirija ya uzazi yako
Unatapika na huwezi kumeza dawa
Ikiwa unatumia dawa ili kutibu PID, usishiriki katika ngono hadi haya mambo 2 yafanyike:
Umemaliza kukunywa dawa zako
Daktari anasema kuwa maambukizi yameisha
Unapotumia dawa zako, waulize watu ambao umeshiriki ngono nao hivi karibuni wapimwe kisonono na klamidia
Ninawezaje kuzuia PID?
Hauwezi kuzuia PID kila mara, lakini ili kupunguza hatari:
Fanya ngono na mpenzi mmoja pekee
Tumia kondomu na dawa za manii wakati wa ngono