Vaginitisi ya Bakteria (BV)

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Je, uke ni nini?

Uke wako huunganisha uterasi yako (utumbo wa mtoto ukiwa mjamzito) na sehemu ya nje ya mwili wako. Pia inajulikana kama njia ya kujifungua. Kuma ni sehemu iliyo katikati ya miguu yako upande wa nje ya mwili wako. Watu wengi hukosea kati ya uke na kuma.

Vaginitisi ya bakteria (BV) ni nini?

BV ni maambukizi ya kawaida sana ya uke ambayo hufanyika wakati bakteria nzuri na mbaya (vijidudu) kwenye uke wako hazina msawazisho. Kwa kawaida uke wako una aina nyingi za bakteria ndani yake. Nyingi ni bakteria nzuri. Bakteria nzuri husaidia kuweka uke wako ukiwa wenye afya kwa kuwekea kikomo kukua kwa bakteria mbaya. Ikiwa una BV, kiwango cha bakteria nzuri hupungua na kiwango cha bakteria mbaya huongezeka.

  • Una uwezekano mkubwa wa vitu kutoka ukeni (kiowevu kizito kutoka kwenye uke wako) ambavyo ni vya rangi ya kijivu au nyeupe na kinatoa harufu ya samaki

  • Kwa kawaida BV huisha siku chache baada ya kuanzia matibabu lakini mara nyingi hurudi

  • Isipotibiwa, BV inaweza kusababisha matatizo makali ya afya (kama vile ugonjwa wa kuchochewa kwa fupanyonga) na magonjwa ikiwa wewe ni mjamzito

Ni nini husababisha BV?

BV inasababishwa na badiliko katika kiwango cha bakteria tofauti kwenye uke wako. Hakuna anayejua ni nini husababisha badiliko hilo au kama tatizo linaweza kutokana na kushiriki ngono. Unaweza kupata BV hata kama haujawahi kushiriki ngono. Lakini ni ya kawaida zaidi ikiwa:

  • Una STI (maambukizi ya zinaa)

  • Una washiriki kadhaa wa ngono

  • Unatumia IUD (kifaa cha intrauterine) kudhibiti uzazi

Dalili za BV ni zipi?

Dalili kuu ni:

  • Vitu vyepesi kutoka ukeni ambavyo ni vya rangi ya kijuvu au vyeupe

  • Kutoka vitu vinavyotoa harufu ya samaki—harufu hii inaweza kuwa kali baada ya kushiriki ngono na wakati wa hedhi yako ya kila mwezi

  • Kuwasha

Daktari wangu anawezaje kujua kama nina BV?

Daktari wako atashuku BV kulingana na dalili zako. Ili kuthibitisha, daktari wako atafanya uchunguzi wa fupanyonga. Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, kwanza daktari wako huangalia uke wako na kisha huangalia ndani ya uke wako. Ili kuangalia sehemu ya ndani, daktari wako atafungua uke wako kwa kifaa kidogo kinachoitwa spekulumu. Daktari wako atachukua sampuli ya kitu kinachotoka kwenye uke wako (ukiwa kuna choochote) ili kukifanyia kipimo.

Madaktari hutibu BV aje?

  • Ikiwa wewe si mjamzito, madaktari watakuandikia dawa za kumeza za kuua bakteria

  • Ikiwa uko mjamzito, madaktari watakuandikia krimu au mafupa yenye dawa ya kuweka kwenye uke wako

  • Maambukizi yakirejea, unaweza kuhitaji kutumia dawa kwa muda mrefu

Mbinu yako ya kudhibiti uzazi huenda isifanye kazi wakati unatibiwa. Baadhi ya krimu zenye dawa zinazotumiwa kutibu BV kufanya kondomu na kizuia mimba kiwe dhaifu.