Trikomoniasisi ya Uke

(Trikomonasi)

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Trikomoniasisi ya uke ni nini?

Trikomoniasisi ya uke ni maambukizi kwenye uke wako. Uke wako huunganisha uterasi yako (utumbo wa mtoto ukiwa mjamzito) na sehemu ya nje ya mwili wako. Pia inajulikana kama njia ya kujifungua. Kuma ni sehemu iliyo katikati ya miguu yako upande wa nje ya mwili wako. Watu wengi hukosea kati ya uke na kuma.

  • Mara kwa mara husababishwa na kushiriki ngono na mwenzi aliyeambukizwa

  • Maambukizi hayo yanaweza kuwa mwilini mwako kwa wiki au miezi kabla upate dalili zozote

  • Unapopata dalili hizi, unaweza kupata vitu kutoka ukeni ambavyo vina rangi ya kijani au manjano (majimaji mazito ambayo hutoka kwenye uke wako) ambacho kinafanana mapovu au kunuka kama samaki—ikiwa hili litatokea, mwone daktari wako

  • Trikomoniasisi ya uke ambayo haijatibiwa inaweza kusababisha matatizo makali, haswa ukipata maambukizi haya wakati uko mjamzito

  • Ili kusaidia kuzuia maambukizi haya, usishiki katika ngono au ukishiriki katika ngono, tumia kondomu

Internal Female Reproductive Anatomy

Ni nini husababisha Trikomoniasisi ya uke?

Unapata trikomoniasisi ya uke kwa kushiriki ngono na mtu ambaye ako nayo. Mwenzi wako anaweza asiwe na dalili zozote za trikomoniasisi ya uke lakini bado anaweza kukuambukiza.

Dalili za trikomoniasisi ya uke ni zipi?

Dalili kuu ni vitu kutoka ukeni ambavyo:

  • Ni vya rangi ya manjano au kijani

  • Agalia kama ina kiputo au povu

  • Vinanukia samaki

  • Vinatoka kwa viwango vikubwa

Huenda pia:

  • Mwasho, wekundu, au maumivu kwenye uke wako

  • Uchungu wakati wa ngono au wakati unapokojoa (kutoa mkojo)

Daktari wangu atajua vipi kuwa nina trikomoniasisi ya uke?

Daktari wako atashuku trikomoniasisi ya uke kulingana na dalili zako. Ili kuthibitisha, daktari wako atafanya uchunguzi wa fupanyonga. Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, daktari wako huchunguza kuma yako na sehemu za ndani za uke wako. Ili kuangalia sehemu ya ndani, daktari wako atafungua uke wako kwa kifaa kidogo kinachoitwa spekulumu. Wakati wa uchunguzi, daktari atatumia kipande cha pamba kuchukua sampuli ya kitu kinachotoka kwenye uke wako na kukipima.

Madaktari hutibuje trikomoniasisi ya uke aje?

  • Utaandikiwa dawa za kuua bakteria za kumeza

  • Hupaswi kunywa pombe kwa angalau saa 72 baada ya kumeza dawa za kuua bakteria—inaweza kukufanya ujihisi mgonjwa, kutapika, na kuwa na maumivu ya kichwa

  • Madaktari watakuambia pia utumie kondomu wakati wa ngono au kutoshiriki katika ngono hadi maambukizi yako yaishe

Wenzi wako wa ngono wanapaswa kuchunguzwa na daktari, ambaye atawaandikia dawa za kuua bakteria sawa. Kwa kawaida wanaume wanahitaji kutumia dawa ya kuua bakteria kwa wiki 1.

Ninawezaje kuzuia trikomoniasisi ya uke?

Ili kupunguza hatari ya kupata maambukizi, tumia kondomu kila mara unaposhiriki ngono.