Maambukizi ya Kuvu Ukeni (Kandidiasi)

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023 | Imebadilishwa Jun 2024

Maambukizi ya kuvu ukeni ni nini?

Chachu inayoitwa Candida ni aina ya kuvu. Baadhi ya Candida zinaishi kwenye uke wako wakati wote. Uke wako huunganisha uterasi yako (utumbo wa mtoto ukiwa mjamzito) na sehemu ya nje ya mwili wako. Pia inajulikana kama njia ya kujifungua. Maambukizi ya kuvu ukeni yanafanyika wakati seli nyingi mno za chachu zinakua kwenye uke wako.

  • Maambukizi haya ni ya kawaida sana na kwa kawaida hayakuwangi kali

  • Maambukizi ya chachu ni ya kawaida sana wakati uko mjamzito, una kisukari, au unatumia dawa za kuua bakteria

  • Dalili zinaweza kuwa mbaya zaidi wiki iliyotangulia hedhi yako ya kila mwezi kuanzia na zinajumuisha mwasho kwenye uke na vitu kutoka

  • Dawa za kuvu zinatumiwa kutibu maambukizi ya chachu

Anatomia ya Ndani ya Uzazi ya Mwanamke

Dalili za maambukizi ya chachu ni zipi?

  • Kuwashwa kwenye uke au kuma yako (sehemu iliyo nje ya mwili wako katika uwazi wa uke wako)

  • Vitu kutoka ukeni vilivyo vizito, vyeupe, vinavyokaa magandi

Dalili zinaweza kuwa mbaya zaidi wiki iliyotangulia hedhi yako ya kila mwezi kuanzia.

Je, daktari wangu anawezaje kujua ikiwa nina maambukizi ya chachu?

Daktari wangu atashuku kuwa una maambukizi ya chachu kulingana na dalili zako. Ili kuthibitisha, daktari wako atafanya uchunguzi wa fupanyonga. Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, daktari wako huchunguza kuma yako na sehemu za ndani za uke wako. Ili kuangalia sehemu ya ndani, daktari wako atafungua uke wako kwa kifaa kidogo kinachoitwa spekulumu. Wakati wa uchunguzi, daktari wako atatumia kipande cha pamba kuchukua sampuli ya kitu kinachotoka kwenye uke wako na kukipima.

Je, maambukizi ya kuvu hutibiwa vipi?

Maambukizi ya chachu yanatibiwa kwa kutumia dawa za kuvu. Hizi zinapatikana kama:

  • Krimu, dawa ya kupaka au mishumaa unayoweka kwenye uke wako (unaweza kupata hizi bila kuandikiwa na daktari)

  • Tembe za kuandikiwa na daktari za kumeza

Mafuta yaliyo kwenye dawa ya kupaka na krimu ya kuvu inaweza kufanya kondomu iliyotengenezwa na ulimbo wa mpira kuwa dhaifu. Ikiwa unapanga kushiriki ngono huku ukitumia mojawapo ya dawa hizi, tumia muundo tofauti wa udhibiti wa uzazi, kama kizuia mimba, lakini pia tumia kondomu ili kuzuia maambukizi ya zinaa (STI).

Ikiwa una hatari ya juu ya kupata maambukizi ya chachu, unaweza kuhitaji kutumia dawa ya kuvu kwa kumeza ili kuzizuia. Kuhitaji kutumia dawa za kuua bakteria kwa muda mrefu kunakuweka katika hatari ya juu ya maambukizi ya chachu.