Vitu kutoka ukeni ni nini?
Vitu kutoka ukeni ni kiowevu kinachotoka kwenye uke wako (njia ya uzazi).
Je, hali ya vitu kutoka ukeni ni hali ya kawaida?
Wanawake wote hutokwa na vitu ukeni wakati mwingine. Kitu cha kawaida kinachotoka ukeni kina rangi nyeupe ya mazima au nyepesi na safi, bila harufu yoyote.
Ni wakati gani ambapo kitu kutoka ukeni huchukuliwa kuwa si cha kawaida?
Kitu kinachotoka ukeni si cha kawaida ikiwa ni:
Kizito au kizito kuliko kawaida
Cheupe na kina bonge (kama jibini ya pamba)
Chenye rangi ya kijivu, kijani, manjano au kinachokaa damu kiasi
Chenye kutoa harufu, kama samaki
Ukiwa na kitu kinachotoka ukeni kisicho cha kawaida, unaweza pia kuwa na mwasho, kuchomwa, upele au maumivu kwenye kuma yako (sehemu iliyo nje ya uwazi wa uke).
Je, napaswa kumwona daktari lini?
Nenda kwa daktari ndani ya siku ikiwa unatoka vitu ukeni na yoyote ya ishara hizi za onyo:
Maumivu ya fupanyonga
Kitu kutoka kinachofanana na usaha
Homa
Kinyesi (mavi) kwenye vitu vinavyotoka ukeni wako
Kutoka vitu vinavyokaa damu baada ya ukomo wa hedhi
Mtoto aliye na homa au kitu kinachotoka chenye rangi ya manjano au kijani ambacho kinatoa harufu inayonukia kama samaki anaweza kuwa na STI (maambukizi ya zinaa), kwa uwezekano kutokana na kudhulimiwa kimwili. Mpeleke mtoto huyu kwa daktari siku hio.
Nenda kwa daktari ndani ya siku chache ikiwa unatoka vitu ukeni visivyo vya kawaida lakini hakuna ishara za onyo.
Maambukizi ya chachu
Ikiwa umekuwa na maambukizi ya chachu hapo awali, hauhitaji kuona daktari kila wakati una dalili za kawaida, isipokuwa kama una dalili zingine pia. Dalili za kawaida ni kutoka kwa vitu vyenye mabonge, vyeupe, vizito na mwasho na kuchomwa kwenye kuma yako. Maambukizi ya chachu yanapaswa kutibiwa kwa dawa za kuvu.
Je, nitarajie nini nikienda kwa daktari?
Madaktari watauliza maswali kuhusu hali yako ya vitu kutoka ukeni na dalili zingine zozote.
Kawaida daktari hufanya uchunguzi wa fupanyonga. Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, daktari wako huchunguza sehemu ya ndani ya uke wako kwa kuufungua akitumia kifaa kidogo kinachoitwa spekulumu. Madaktari wanaweza kutumia swab ya pamba ili kuchukua sampuli ya kitu kinachotoka ili kufanyiwa kipimo.
Madaktari hutibu hali ya vitu kutoka ukeni isiyo ya kawaida vipi?
Madaktari wanatibu kisababishaji cha vitu kutoka kwako, ikiwa wanaweza. Kwa mfano, ikiwa una maambukizi yanayosababishwa na bakteria, madaktari watakupatia dawa za kuua bakteria za kumeza.
Ikiwa unahisi uchungu na mwasho, madaktari wanaweza pia kukupendekezea:
Dumisha usafi wa uke wako kadri iwezekanavyo
Wekelea barafu kwenye uke wako
Lowesha kwenye maji vuguvugu
Usitumie krimu, poda, sabuni wala vitu vingine vinavyosababisha mwasho kwenye uke wako
Dawa za kupaka (kama vile krimu ya kotikosteroidi)