Kutokwa na Damu Ukeni

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Kutoka damu ukeni ni nini?

Kutoka damu ukeni ni wakati anbapo unapitisha damu kutoka kwenye uke wako (njia ya uzazi).

Je, kutokwa damu ukeni ni kawaida?

Wakati mwingine ndiyo na wakati mwingine sio. Kuvuja damu ukeni ni kwa kawaida wakati wa hedhi yako ya kila mwezi. Hedhi yako kwa kawaida huanzia baada ya kila siku 21 hadi 35 (au hadi siku 45 kwa vijana) Kwa kawaida kutoka damu wakati wa hedhi kunadumu kwa siku 3 hadi 7. Kwa kawaida wasichana hupata hedhi yao ya kwanza wakati wana umri wa kati ya miaka 10 na 16.

Watoto wasichana waliozaliwa hivi karibuni wanaweza kuvuja damu ukeni kwa hadi wiki 2 baada ya kuzaliwa—hii ni ya kawaida pia. Kuvuja damu kukiendelea kwa wasichana waliozaliwa karibuni kwa zaidi ya wiki 2, wanapaswa kupelekwa kwa daktari.

Ni wakati gani ambapo kuvuja damu ukeni huwa ni hali ya kawaida?

Kutokwa damu huchukuliwa kuwa hali isiyo ya kawaida pale unapovuja damu:

  • Kabla upate hedhi yako ya kwanza

  • Katikati mwa hedhi zako

  • Wakati uko mjamzito

  • Baada ya kuacha kupata hedhi (ukomo wa hedhi)

Kuvuja damu wakati wa hedhi yako kunaweza pia kuchukuliwa kuwa jambo lisilo la kawaida ikiwa hedhi yako:

  • Inadumu zaidi ya siku 7

  • Ni nzito mno (unatumia zaidi ya kisodo au padi 1 au 2 kwa saa)

  • Inatokea mara nyingi (kuanzia chini ya siku 21 baada ya nyingine)

  • Inatokea mara nyingi (kuanzia zaidi ya siku 90 baada ya nyingine)

Je, kutokwa damu ukeni isivyo kawaida ni hali ya hatari?

Kunaweza kuwa na madhara zaidi ikiwa unavuja damu nyingi. Inaweza kuwa mbaya zaidi hata kama hakuna kuvuja damu nyingi zaidi lakini kisababishaji kina madhara zaidi (kwa mfano, saratani).

Ikiwa unavuja damu ambako kunadumu kwa muda mrefu, kiwango chako cha damu kitapungua (anemia). Anemia hukufanya ukae mwenye kupauka na kuhisi kuchoka wakati wote. Mwili wako pia utakuwa na kiwango cha chini cha madini chuma, kwa sababu seli nyekundu za damu zina madini chuma ndani yake. Ikiwa unavuja damu nyingi kwa wakati mmoja, shinikizo lako la damu linaweza huwa chini kupita kiasi (hali inayoitwa mshtuko) na unaweza kuzirai.

Ni nini husababisha kuvuja damu ukeni?

Visababishaji vya kawaida vya kuvuja damu kusio kwa kawaida kunategemea umri wako.

Wasichana wadogo wanaweza kuumizwa au kuwa na kitu kimekwama kwenye uke wao, kama vile karatasi ya choo au mwanasesere. Wasichana walio na chini ya umri wa miaka 8 wanaweza kuanzia kubalehe mapema zaidi. Kudhulumiwa kimwili kunaweza pia kusababisha kuvuja damu ukeni.

Wasichana ambao wanaanzia tu tupata hedhi au wanawake ambao wanamalizia tu hedhi zao wanaweza kuwa na kuvuja damu kusio kwa kawaida kwa sababu ya mabadiliko katika homoni zao. Baadhi ya wasichana au wanawake wanaweza kuwa na tatizo walilorithi la kuganda kwa damu.

Wanawake wenye umri mdogo na wa kati wanaweza kuwa na:

  • Matatizo ya ujauzito (kuharibika mimba, ujauzito katika sehemu isiyofaa [ujauzito wa nje ya kizazi])

  • Fibroidi (uvimbe kwenye uterasi ambao unaweza kuwa na maumivu lakini hausababishi saratani)

  • Kutokwa na matone ya damu kwenye uke kwa sababu ya dawa ya kuzuia mimba

Kwa wanawake wazee ambao hawapati hedhi tena, kuvuja damu kunaweza kusababishwa na matatizo ya homoni au saratani.

Je, napaswa kumwona daktari lini?

Nenda kwa daktari mara moja ikiwa unavuja damu ukeni na una yoyote kati ya ishara hizi za onyo:

  • Kuzirai, udhaifu, kizunguzungu, mafua na ngozi yenye jasho, tatizo katika kupumua au mdundo wa moyo ambao ni hafifu au wa haraka zaidi

  • Kuvuja damu wakati wa ujauzito

  • Kuvuja damu sana wakati wa hedhi yako—kutumia zaidi ya padi au kisodo 1 kwa saa kwa saa chache

  • Kutoa damu iliyoganda au mabonge makubwa ya tishu

Unapaswa kwenda kwa daktari mara moja ikiwa una ishara za tatizo la kutokwa na damu:

  • Unavilia kwa urahisi

  • Unavuja damu sana unapopiga meno mswaki au unapokatwa kidogo

  • Una madoa madogo yenye rangi nyekundu-zambarau au madoa makubwa zaidi kwenye ngozi yako

Nenda kwa daktari ndani ya wiki ikiwa hauna ishara zozote za onyo lakini una kuvuja damu kusio kwa kawaida, ikijumuisha ikiwa una kuvuja damu ukeni kabla ya kipindi chako cha hedhi kuanzia (kabla ya ubalehe) au baada ya kuacha (baada ya ukomo wa hedhi).

Mtoto msichana aliyezaliwa hivi karibuni anayevuja damu kwa zaidi ya wiki 2 anafaa kwenda kwa daktari.

Je, nitarajie nini nikienda kwa daktari?

Madaktari watauliza maswali kuhusu kuvuja damu ukeni kwako, dalili zingine na hedhi yako ya kawaida ya kila mwezi.

Kawaida daktari hufanya uchunguzi wa fupanyonga. Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, daktari wako huangalia ndani ya uke na mlango wa kizazi (sehemu ya chini ya uterasi yako). Ili kuangalia sehemu ya ndani, daktari wako atafungua uke wako kwa kifaa kidogo kinachoitwa spekulumu.

Wanaweza kufanya kipimo cha ujauzito cha mkojo, vipimo vya damu na pengine kipimo kwa kutumia mawimbi ya sauti (kwa kutumia mawimbi ya sauti kuunda picha zinazosonga za sehemu ya ndani ya sehemu yako ya fupanyonga).

Madaktari hutibu aje kuvuja damu ukeni kusio kwa kawaida?

Madaktari watatibu chanzo kinachosababisha uvuje damu. Kwa mfano, ikiwa una uvimbe au kishikizo kingine, madaktari wanaweza kufanya upasuaji ili kukitoa.

Ikiwa kuvuja damu kumesababisha uwe na kiwango kidogo sana cha madini chuma kwenye damu yako, unaweza kuhitaji kumeza tembe za madini chuma.

Ikiwa umepoteza kiwango kikubwa sana cha damu chote kwa wakati mmoja na uko kwa mshtuko, madaktari watakupatia viowevu vya IV au kuongezewa damu (kiowevu au damu ambayo inaingia moja kwa moja kwenye mshipa wako wa damu). Hii itasaidia kupandisha shinikizo lako la damu.