Uvimbe kwenye Uterasi

(Leiomyomas; myoma)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2023

Je, uvimbe kwenye uterasi ni nini?

Uvimbe kwenye uterasi ni uvimbe uliopo kwenye uterasi ya mwanamke (mfuko wa uzazi). Uterasi ni kiungo ambacho watoto hukua kabla ya kuzaliwa. Fibroidi sio saratani, lakini inaweza kuwa na maumivu makali na kusababisha uvujaji wa damu na dalili nyingine.

  • Fibroidi zinahitaji matibabu ikiwa zinasababisha dalili tu—fibroidi nyingi hazihitaji matibabu

  • Hadi wanawake 7 kati ya 10 Wazungu na 8 kati ya 10 ya wanawake weusi huwa na uvimbe mmoja au zaidi kwenye mfuko wa uzazi wanapofikisha umri wa miaka 45

  • Uvimbe kwenye uterasi zinaweza kuwa ndogo au kubwa kama mpira wa vikapu

  • Madaktari huchunguza vimbe kwenye mfuko wa uzazi kwa kutumia uchunguzi wa mwili na upigaji picha kutumia mawimbi ya sauti (kipimo cha kutumia mawimbi ya sauti kuunda picha inayosonga ya ndani ya mwili wako)

  • Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi huwapata zaidi wanawake ambao wana uzani wa kupita kiasi

  • Unaweza kuhitaji upasuaji ili kuondoa dalili kama vile maumivu au kukuwezesha kuzaa

Je, uvimbe wa mfuko wa uzazi husababishwa na nini?

Madaktari hawajui chanzo cha uvimbe kwenye mfuko wa uzazi.

Viwango vya juu vya homoni za kike ya estrojeni na projesteroni hufanya uvimbe kwenye mfuko wa uzazi kuongezeka. Mara nyingi uvimbe huzidi kukua kubwa wakati viwango vya homoni hizi vinapopanda wakati wa ujauzito. Mara nyingi hupungua wakati viwango hivi vya homoni vinapungua wakati wa ukomo wa hedhi.

Je, dalili za uvimbe kwenye mfuko wa uzazi ni zipi?

Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi mwingi hausababishi dalili zozote. Dalili zako zinaweza kutegemea:

  • Idadi ya uvimbe ulio nao kwenye mfuko wa uzazi

  • Mahali zilipo kwenye uterasi yako

  • Ukubwa (uvimbe mkubwa zaidi kwenye mfuko wa uzazi unaweza kusababisha dalili)

Dalili za uvimbe kwenye mfuko wa uzazi zinaweza kujumuisha:

  • Kuvuja damu nyingi zaidi wakati wa kipindi chako cha hedhi au kuwa kipindi kirefu cha hedhi (uvujaji wa damu ukeni usio wa kawaida)

  • Anemia (idadi ndogo ya seli nyekundu za damu) kutokana na kutokwa na damu nyingi wakati wa hedhi

  • Maumivu, shinikizo, au hisia ya uzito katika sehemu ya chini ya tumbo lako

  • Haja ya mara kwa mara au ya ghafla ya kukojoa

  • Kufunga choo (ugumu wa kutoa kinyesi)

  • Ugumu wa kukojoa

  • Sehemu ya tumbo iliyovimba

Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi unaweza pia kusababisha matatizo kwa ujauzito kama vile:

  • Matatizo ya kupata ujauzito

  • Kuharibika kwa mimba (ujauzito wako unapokoma kabla ya wiki ya 20, kabla ya mtoto wako kuwa na uwezo wa kuishi nje ya mwili wako)

  • Kupata uchungu wa uzazi mapema sana

  • Nafasi isiyo ya kawaida ya mtoto kwenye uterasi

  • Kupoteza damu nyingi sana baada ya kujifungua (kuvuja damu baada ya kujifungua)

Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi unaweza kukua mkubwa na kushindwa kupata damu ya kutosha. Hii inawafanya kupungua na kukusababishia maumivu.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina uvimbe kwenye mfuko wa uzazi?

Madaktari watafanya uchunguzi wa fupanyonga na wanaweza kupendekeza vipimo vingine. Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, daktari wako anafinya tumbo lako ili kuhisi ukubwa na umbo la uterasi na ovari zako. Wanatumia pia zana kuangalia ndani ya uke wako na mlango wa kizazi (sehemu ya chini ya uterasi yako) ili kuchunguza matatizo yoyote.

Ili kujua kwa uhakika kama una uvimbe kwenye mfuko wa uzazi, madaktari wanaweza kufanya vipimo vingine ikiwa ni pamoja na:

  • Kipmo cha kupiga picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa kutumia kifaa kilichowekwa ndani ya uke wako (upigaji picha kwa kutumia mawimbi ya sauti ya transvaginal)

  • Kipimo cha kupiga picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kinafanywa baada ya daktari kuingiza kiowevu kwenye uterasi yako ili kuona ndani

  • MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku)—kipimo cha upigaji wa picha kinachotumia mawimbi thabiti ya sumaku kuunda picha yenye maelezo ya kina ya ndani ya mwili wako

  • Uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi wa utando wa uterasi yako

Katika uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi, daktari huondoa kiasi kidogo cha tishu kutoka kwenye utando wa uterasi yako. Tishu huchunguzwa kwa darubini ili kuhakikisha kuwa huna tatizo kubwa zaidi, kama vile saratani ya uterasi.

Je, madaktari hutibu vipi uvimbe kwenye mfuko wa uzazi?

Hautahitaji matibabu isipokuwa ikiwa dalili zako zitakusumbua au zikuzuie kupata ujauzito. Ikiwa uvimbe kwenye mfuko wa uzazi wako utakuwa mkubwa au ukianza kusababisha dalili kali, matibabu yanaweza kujumuisha:

  • Dawa za kupunguza uvimbe kwenye mfuko wa uzazi na kupunguza kuvuja damu

  • Wakati mwingine, upasuaji ili kuondoa uvimbe kwenye mfuko wa uzazi wako au uterasi yako

  • Wakati mwingine, taratibu za kuharibu uvimbe ulionao kwenye mfuko wa uzazi na kupunguza dalili zako

Taratibu zinazoweza kuharibu uvimbe kwenye mfuko wa uzazi ni pamoja na kuzigandisha au kutumia joto. Kipimo cha kupiga picha kwa kutumia mawimbi ya sauti au MRI inaweza kutumika wakati wa utaratibu ili kumsaidia daktari wako kuona uvimbe kwenye mfuko wa uzazi.

Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi unaweza kusinyaa zenyewe baada ya ukomo wa hedhi.