Kutokwa Na Damu Nyingi Kwa Uterasi wakati wa Kujifungua

(Kuvuja Damu Baada ya Kujifungua)

Imepitiwa/Imerekebishwa Sept 2023

Uterasi kuvuja damu kupita kiasi ni nini?

Hali fulani ya kuvuja damu baada ya kujifungua ni kawaida. Zaidi ya vikombe 4 (zaidi ya mL 1000) vya damu iliyovuja baada ya kujifungua kwa njia ya uke ni uterasi kuvuja damu kupita kiasi.

  • Sababu iliyozoeleka inayosababisha kuvuja damu kupita kiasi ni uterasi yako kuvutika na haibani (kunywea) kama inavyopaswa kuwa

  • Madaktari wanatibu hali hii ya kuvuja damu kupita kiasi kwa kuchua tumbo lako na kukupa dawa ili kusaidia uterasi yako kukaza

  • Madaktari wanaweza kukuongezea damu

  • Nadra sana utahitaji kufanyiwa upasuaji

Ni nini kinachosababisha kuvuja damu wakati wa kujifungua?

Mara nyingi, unatokwa na damu nyingi kwa sababu:

  • Uterasi yako haikazi baada ya kujifungua kama inavyopaswa kuwa

Sababu nyingine za kuvuja damu sana, zinajumuisha:

  • Shingo ya uzazi (sehemu ya chini ya uterasi yako) ilichanika wakati wa kujifungua

  • Tatizo la kutokwa na damu ambalo linafanya damu yako isigande

  • Sehemu ya kondo lako la nyuma (baada ya kujifungua) ilibaki ndani ya uterasi yako baada ya kujifungua

Una hatari kubwa ya kuvuja damu ikiwa:

  • Umezaa watoto wengi sana

  • Ulipata uchungu wa uzazi kwa muda mrefu

  • Ulijifungua zaidi ya mtoto mmoja (kama vile mapacha au mapacha watatu)

  • Umejifungua mtoto mkubwa sana

Madaktari wanaweza kufanya nini ili kunisaidia nisivuje damu kupita kiasi?

Kabla hujapata uchungu, madaktari wanachukua hatua kuzuia au kujiandaa kwa ajili ya hali ya kuvuja damu baada ya kujifungua.

  • Wanaweza kuangalia hatari za kuvuja damu, kama vile kuwa na maji mengi ya amnioti au ugonjwa wa kutokwa na damu

  • Ikiwa una aina ya damu isiyo ya kawaida, madaktari wanahakikisha kuwa aina ya damu yako inapatikana

  • Wanajaribu kumzalisha mtoto wako taratibu kadiri inavyowezekana

  • Baada ya kujifungua, madaktari wanakuangalia kwa angalau saa 1, wanahakikisha kwamba uterasi yako imekaza na kuangalia kama damu inavuja

Madaktari watajuaje ikiwa ninatoka damu kupita kiasi?

Madaktari watafanya:

  • Wataangalia ikiwa kuna damu nyingi inayovuja

  • Watabonyeza kwenye eneo la tumbo lako kuona ikiwa uterasi imekaza kama inavyotakiwa

  • Kuangalia shinikizo la damu yako na kasi ya mapigo ya moyo wako, kupungua kwa shinikizo la damu au mapigo ya moyo ya haraka yanaweza kumaanisha unapoteza damu nyingi

Nini kinachotokea ikiwa nitaanza kuvuja damu sana?

Madaktari watafanya:

  • Kandamiza kwa nguvu na uchue tumbo lako uli kusaidia uterasi yako ikaze

  • Kuangalia kwenye uke wako na shingo ya uzazi ikiwa kuna hali ya kuchanika

  • Watakupa dawa ili kufanya uterasi yako ikaze

  • Watakupatia majimaji au damu kupitia mishipa yako ili kufidia damu iliyopotea

Kukandamiza tumbo lako kunasaidia uterasi kukaza na kuzuia kuvuja damu. Kuna dawa kadaa tofuati ambazo madaktari wanaweza kutoa kwenye IV au kama sindano kwenye mkono wako.

Ikiwa kuvuja damu kutaendelea, madaktari wanaweza kufanya upasuaji ikiwa ni pamoja na:

  • Kuangalia ndani ya uterasi yako ili kuondoa mabaki yoyote ya kondo la nyuma yaliyosalia (baada ya kujifungua)

  • Kuweka puto ndani ya uterasi yako ili kukata mtiririko wa damu

  • Kufungasha ndani ya uterasi yako kwa kutumia gozi

  • Kushona kwa kuzunguka sehemu ya chini ya uterasi

  • Kuziba mishipa mikubwa ambayo inaleta damu kwenye uterasi yako

  • Kama hatua ya mwisho, histerektomia (kuondoa uterasi yako)