Mwasho wa sehemu za uzazi

(Mwasho kwenye Uke; Kuwashwa kwenye Kuma)

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Mwasho wa sehemu za uzazi ni nini?

Mwasho wa sehemu za uzazi ni wakati uke wako (njia ya uzazi) au sehemu iliyo nje ya mdomo wa uke (inayoitwa valva) inahisi kukunwa na kuwasha.

Wanawake wengi wana mwasho wa sehemu za uzazi mara moja baada ya muda ambao huisha wenyewe.

Mwasho wa sehemu za uzazi ni tatizo isiyoisha yenyewe au kuendelea kurudi. Mwasho wa sehemu za uzazi unaweza kuwa na madhara ikiwa pia una:

Nini husababisha mwasho wa sehemu za uzazi?

Je, napaswa kumwona daktari lini?

Nenda kwa daktari mara moja ikiwa una mwasho wa sehemu za uzazi na maumivu ya fupanyonga au vitu kutoka ukeni visivyo vya kawaida. Nenda kwa daktari wakati unaweza ikiwa mwasho kwako kunadumu zaidi ya siku chache lakini hauna maumivu au vitu kutoka ukeni visivyo vya kawaida.

Je, nitarajie nini nikienda kwa daktari?

Madaktari watauliza maswali kuhusu mwasho wa sehemu za uzazi na dalili zingine zozote.

Kawaida daktari hufanya uchunguzi wa fupanyonga. Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, daktari wako huchunguza sehemu ya ndani ya uke wako kwa kuufungua akitumia kifaa kidogo kinachoitwa spekulumu. Madaktari wanaweza kupangusa kwa kutumia pamba ili kuchukua sampuli ya vitu vyovyote vinavyotoka ukeni (kiowevu) ili kufanya vipimo.

Madaktari hutibu vipi mwasho wa sehemu za uzazi?

Madaktari wanatibu kisababishaji cha mwasho wako, ikiwa wanaweza. Kwa mfano, ikiwa una maambukizi ya chachu, madaktari wanaweza kukupea dawa za kuvu.

Wanaweza pia wakakupendekezea:

  • Dumisha usafi wa uke wako kadri iwezekanavyo

  • Wekelea barafu kwenye uke wako

  • Lowesha kwenye maji vuguvugu

  • Usitumie krimu, poda, sabuni wala vitu vingine vinavyosababisha mwasho kwenye uke wako

Ikiwa mwasho wako hautaisha, madaktari wanaweza kupendekeza dawa (kama vile krimu ya kotikosteroidi).