Kuvimba kwa mlango wa kizazi

Imepitiwa/Imerekebishwa Apr 2023

Je, shingo ya kizazi ni nini?

Mlango wako wa kizazi ni sehemu ya chini ya uterasi yako katika sehemu ya juu ya uke wako. Uke wako huunganisha uterasi yako (utumbo wa mtoto ukiwa mjamzito) na sehemu ya nje ya mwili wako.

Kuvimba kwa mlango wa kizazi ni nini?

Kuvimba kwa mlango wa kizazi ni wakati mlango wa kizazi unawashwa.

  • Kwa kawaida kisababishaji huwa ni STI (maambukizi ya zinaa)

  • Huenda usiwe na dalili zozote au unaweza kutokwa na kitu (kiowevu kizito) na kuvuja damu kutoka kwenye uke wako

  • Ikiwa unatoa kitu kinachokaa usaha au cha rangi ya manjano-kijani, kuvuja damu ambako si sehemu ya hedhi yako ya kila mwezi au uchungu wakati wa ngon, ona daktari wako

  • Kwa kawaida madaktari watakuandikia dawa za kuua bakteria

  • Kuvimba kwa mlango wa kizazi kusikotibiwa kunaweza kuenea na kudhuru sehemu nyingine ya uterasi yako

Anatomia ya Ndani ya Uzazi ya Mwanamke

Ni nini husababisha kuvimba kwa mlango wa kizazi?

Maambukizi yanayosababisha kuvimba kwa mlango wa kizazi

Wakati mwingine maambukizi ya uke, kama vile vaginitisi ya bakteria na trikomoniasisi pia yanaathiri mlango wa kizazi.

Visababishaji vingine vya kuvimba kwa mlango wa kizazi

  • Vitu vilivyoachwa kwenye uke wako kwa muda mrefu sana, kama vile vizuia mimba

  • Kemikali kwenye douche au krimu za kudhibiti uzazi

  • Kutumia kondomu za ulimbo wa mpira, ikiwa una mzio wa ulimbo wa mpira

Dalili za kuvimba kwa mlango wa kizazi ni zipi?

Kuvimba kwa mlango wa kizazi kunaweza kosa kusababisha dalili. Kunaposababisha, unaweza ukawa na:

  • Kutokwa na kitu ukeni ambacho kinaweza kuwa chenye rangi ya manjano-kijani au kinachokaa usaha

  • Kuvuja damu ukeni baina ya hedhi yako ya kila mwezi au baada ya ngono

  • Uchungu wakati wa ngono, wakati wa kukojoa (kutoa mkojo) au zote mbili

  • Uwekundu kando ya mlango wa uke wako

Daktari wangu anawezaje kujua kama nina hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi?

Daktari wako atashuku hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi kulingana na dalili zako. Ili kuthibitisha, daktari wako atafanya uchunguzi wa fupanyonga. Wakati wa uchunguzi wa fupanyonga, daktari wako huchunguza sehemu ya ndani ya uke wako kwa kuufungua akitumia kifaa kidogo kinachoitwa spekulumu. Madaktari watafanya:

  • Kuchukua sampuli ya kitu chochote kinachotoka kwa ajili ya kupima

  • Kugusa mlango wako wa kizazi kwa kutumia kipande cha pamba ili kuona kama unavuja damu kwa urahisi

Daktari wangu atatibuje hali ya kuvimba kwa mlango wa kizazi?

Kwa sababu kisonono na klamidia ndio visababishaji vyenye uwezekano mkubwa wa kusababisha kuvimba kwa mlango wa kizazi, daktari wako atakuandikia dawa za kuua bakteria ili kutibu magonjwa hayo. Kwa kawaida unaweza kumeza hizi nyumbani, lakini unaweza pia kuhitaji sindano.

Daktari wako anaweza kukwambia:

  • Usishiriki ngono hadi umalize dawa yako na maambukizi yako yaishe

  • Kumuuliza mshirika wako wa ngono apimwe STI

Baada ya miezi 3 hadi 6, daktari wako atakupima tena ili kuona kama maambukizi yako yameisha.

Ninawezaje kuzuia kuvimba kwa mlango wa kizazi?

Hauwezi kuzuia kuvimba kwa mlango wa kizazi kila wakati. Ili kupunguza hatari yako:

  • Fanya ngono na mpenzi mmoja pekee

  • Tumia kondomu unaposhiriki ngono