Kibofu cha mkojo chenye nyurojeniki ni nini?
Kibofu chako cha mkojo ni mahali ambapo mkojo unahifadhiwa hadi unapokuwa tayari kukojoa.
Kibofu cha mkojo chenye nyurojeniki ni ukosefu wa uwezo wa kudhibiti kibofu cha mkojo unaosababishwa na matatizo ya neva ambazo zinaelekea kwenye kibofu cha mkojo.
Kibofu chako cha mkojo kinaweza kujaa na hadi mkojo kumwagika nje
Unaweza kuhisi hamu kubwa ya kukojoa hata pale ambapo kibofu chako cha mkojo hakikujaa
Mara nyingi madaktari huondoa mkojo kwenye kibofu chako kwa kutumia katheta mara kadhaa kwa siku
Wakati mwingine, dawa husaidia
Kwa kupata matibabu mara moja kunaweza kuzuia uharibifu wa figo
Baadhi ya matatizo ya neva huzuia misuli ya kibofu chako cha mkojo kukaza kama inavyotakiwa. Kisha kibofu chako cha mkojo hujaa mkojo na wewe kuvuja mkojo. Unapokojoa, kibofu chako cha mkojo hakitoi mkojo wote.
Matatizo mengine ya neva husababisha misuli ya kibofu chako cha mkojo kukaza kupita kiasi au kwa wakati usio sahihi. Hivyo unaweza kukojoa mara kwa mara na kukojoa wakati hutaki kukojoa.
Je, nini husababisha kibofu cha mkojo chenye nyurojeniki?
Dalili za kibofu cha mkojo chenye nyurojeniki ni zipi?
Dalili kuu ni kushindwa kudhibiti ni wakati gani ukojoe (kutoweza kujizuia kukojoa). Ukiwa na kibofu cha mkojo chenye nyurojeniki unaweza kuwa unapitisha kiasi kidogo cha mkojo wakati wote.
Dalili zingine ni pamoja na:
Haja ya kukojoa mara kwa mara na kwa haraka, ikiwa ni pamoja na usiku
Kwa wanaume, upungufu wa nguvu za kiume
Kibofu cha mkojo chenye nyurojeniki kinaongeza hatari yako ya:
Matatizo ya figo kuanzia lile la mkojo kurejea kwenye figo zako
Madaktari wanawezaje kufahamu ikiwa nina kibofu cha mkojo chenye nyurojeniki?
Madaktari hushuku uwepo wa kibofu cha mkojo chenye nyurojeniki ikiwa unapata matatizo ya kudhibiti kukojoa. Watatumia kipimo cha upigaji picha kwa mawimbi ya sauti au katheta ili kupima kiasi cha mkojo kilichobaki katika kibofu chako cha mkojo mara utakapomaliza kukojoa. Daktari pia atafanya vipimo kama vile:
Kipimo cha picha kwa kutumia mawimbi ya sauti kwa njia yako ya mkojo ili kukagua kama kuna uharibifu
Vipimo vya damu ili kukagua utendakazi wa figo
Ikiwa inaonekana kuwa una kibofu cha mkojo chenye nyurojeniki, madaktari wanaweza kufanya vipimo maalum zaidi vya kibofu chako cha mkojo.
Je, madaktari wanatibu vipi kibofu cha mkojo chenye nyurojeniki?
Ikiwa kibofu chako cha mkojo hujaa na kina shida ya kuondoa mkojo wote, madaktari watakufanya:
Utumie katheta kuondoa mkojo wote kwenye kibofu chako cha mkojo mara kadhaa kwa siku
Katheta hufanya mkojo kutiririka hadi chini. Utumie katheta kabla ya kibofu chako cha mkojo kujaa sana kiasi kwamba ukavujisha mkojo. Madaktari wanapendelea kutokuacha katheta wakati wote. Ni bora kuiweka na kuiondoa mara baada ya mkojo kutoka.
Ikiwa kibofu chako cha mkojo kitakaza kwa wakati usio sahihi, madaktari wanaweza:
Dawa
Mbinu za kufunza kibofu cha mkojo na ulegevu
Madaktari watakufanya unywe majimaji mengi wakati wa mchana, ili kuepusha mawe kwenye figo.
Watachunguza ili kuhakikisha kwamba figo zako zinafanya kazi vizuri.