Ugonjwa wa shida ya akili ya Parkinson (PD)

Ugonjwa wa shida ya akili ya Parkinson (PD)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2024

Ugonjwa wa Parkinson ni nini?

Ugonjwa wa Parkinson ni ugonjwa wa ubongo unaosababisha kupoteza udhibiti wa mwendo wako polepole. Inaweza kusababisha kutetemeka (kutetemeka), misuli kukazika, mwendo wa taratibu, na matatizo ya kupoteza usawa. Kwa watu wengi, pia husababisha matatizo ya kufikiri au kupoteza kumbukumbu (kumbukumbu yako na uwezo wako wa kujifunza unazidi kuzorota kadri muda unavyopita).

  • Ugonjwa wa Parkinson hutokea kutokana na uharibifu wa sehemu ya ubongo wako inayoitwa basal ganglia, ambayo husaidia kudhibiti mwendo na usawa

  • Dalili ya kawaida ni kutetemeka (kutetemeka kwa sehemu ya mwili usiyoweza kudhibiti)

  • Hakuna tiba ya ugonjwa wa Parkinson, lakini matibabu yanaweza kusaidia kudhibiti dalili

  • Hatari ya kupata ugonjwa wa Parkinson inaongezeka kadiri umri unavyokuwa mkubwa

Ni nini husababisha ugonjwa wa Parkinson?

Unaposogeza misuli, ishara husafiri kupitia basal ganglia kwenye ubongo wako. Basal ganglia hutengeneza dutu inayoitwa dopamini. Dopamini hurahisisha mwendo. Ugonjwa wa Parkinson huharibu basal ganglia hivyo isiweze kutoa dopamini ya kutosha. Bila dopamini ya kutosha, mwendo wako unaweza kuwa wa taratibu, wenye kushtuka shtuka, au mgumu.

Madaktari hawajui kwa hakika nini husababisha ugonjwa wa Parkinson. Huwa ya kurithi katika familia, kwa hiyo labda kuna sababu ya kijeni.

Magonjwa mengine ya ubongo na dawa fulani au sumu wakati mwingine husababisha dalili zinazofanana na ugonjwa wa Parkinson (hali ya kuwa na ugongwa wa parkinson).

Dalili za ugonjwa wa Parkinson ni nini?

Dalili za kwanza za ugonjwa wa Parkinson kawaida ni:

  • Kutetemeka (mitetemo) ya vidole na mikono wakati misuli yako imelegea na umepumzika—hii ndiyo dalili ya kwanza inayojulikana zaidi.

  • Matatizo ya mwendo — mwendo wako huwa wa taratibu na mgumu kuanza

  • Kupungua kwa hisi ya harufu

Dalili zingine za ugonjwa wa Parkinson ni pamoja na:

  • Misuli yako kuwa migumu na vigumu kusogea.

  • Matatizo ya usawaziko na kutembea, kusimama, au kuketi

  • Matatizo ya kupepesa macho au kumeza

  • Usemi mwepesi, wenye kigugumizi

  • Matatizo ya kulala

  • Matatizo ya kufikiri (kupoteza kumbukumbu)

Madaktari wanawezaje kujua kama nina ugonjwa wa Parkinson?

Madaktari hugundua ugonjwa wa Parkinson kulingana na:

  • Dalili zako na kipimo cha kimwili

  • Vipimo kama vile tomografia ya kompyuta (uchanganuzi wa CT) au upigaji picha kwa mvumo wa sumaku (MRI)

Uchanganuzi wa CT au MRI inaweza kumsaidia daktari kuona ikiwa tatizo lingine la ubongo linasababisha dalili zako.

Madaktari hushughulikia vipi ugonjwa wa Parkinson?

Hakuna tiba ya ugonjwa wa Parkinson.

Madaktari hukutibu kwa:

  • Tiba ya kuzoeza mwili na tiba ya kimazingira

  • Dawa, kama vile levodopa na carbidopa

  • Wakati mwingine upasuaji wa kuweka vielektrodi vidogo katika ubongo wako ili kuchochea basal ganglia (upasuaji unaoitwa kichocheo cha kina cha ubongo)

Tiba ya kimwili na tiba ya shughuli za kila siku zinaweza kukusaidia kuweza kusogea na kujitegemea kwa kadiri inavyowezekana katika shughuli zako za kila siku na kutembea.

Dawa kama vile levodopa na carbidopa zinaweza kurahisisha mwendo na kukuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi kwa miaka mingi.

Madaktari wanaweza kusisimua ubongo kwa kina ikiwa tu una dalili kali na dawa hazisaidii. Katika kusisimua ubongo kwa kina, daktari wako ataweka waya nyembamba kupitia mwanya mdogo kwenye fuvu lako na kisha kwenye eneo la ubongo ambalo lina tatizo. Ncha ile nyingine ya waya hupitia kwenye ngozi yako na kuunganishwa na betri chini ya mtulinga wako. Kifaa hicho hutuma mawimbi ya umeme kwenye maeneo ya ubongo wako ambayo yana matatizo.

Baadhi ya hatua rahisi zinaweza pia kusaidia:

  • Kuendelea kufanya shughuli nyingi iwezekanavyo za kila siku

  • Jishughulishe kwa ratiba ya mara kwa mara

  • Rahisisha kazi za kila siku—kwa mfano, tumia viungio vya Velcro badala ya vifungo kwenye nguo zako na ununue viatu vilivyo na viungio vya Velcro.

  • Tumia vifaa vya usaidizi, kama vile vya kuvuta zipu na kufunga vifungo

  • Ondoa vitu vilivyo sakafuni ili kuzuia kuanguka

  • Weka vyuma vya kujishikilia bafuni na viegemeo kwenye vijia ili kuzuia kuanguka

Wasaidizi na masuala ya mwisho wa maisha

Hatimaye utahitaji usaidizi katika shughuli za kawaida za kila siku, kama vile:

  • Kula

  • Kuoga

  • Kuvaa nguo

  • Kwenda haja

Inaweza kuwa na manufaa sana kwa wasaidizi wakijifunza kuhusu ugonjwa wa Parkinson na njia za kukusaidia. Kazi ya usaidizi inachosha na kufadhaisha, na wasaidizi wengi hunufaika na kujiunga na vikundi vya wasaidizi.

Watu wengi walio na ugonjwa wa Parkinson hushindwa kufanya shughuli za kimsingi, na watu wengi (takriban 1 kati ya 3) hupata ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu. Kabla ya haya kutokea, ni vizuri kuandika maelekezo ya mapema. Maelekezo ya mapema ni mpango ulioandikwa wa kuwajulisha wapendwa wako na madaktari ni aina gani za matibabu ungependa kupata kuelekea mwishoni mwa maisha yako.

Ninaweza kupata wapi habari zaidi kuhusu ugonjwa wa Parkinson?