Ugonjwa wa Huntington ni nini?
Ugonjwa wa Huntington ni ugonjwa wa kijeni unaosababisha kuvunjika polepole kwa seli maalum za neva kwenye ubongo.
Mara nyingi dalili huanza kati ya miaka 35 na 40
Ugonjwa huu huharibu sehemu ya ubongo wako ambayo hukusaidia kusogeza viungo taratibu na katika hali iliyoratibiwa
Mwendo huwa wa taratibu, wenye mitetemeko, na usio na ustadi, na usemi wako hukokoteka.
Utendaji wa akili huathiriwa na unakuwa na mfadhaiko na hasira, na kumbukumbu na kufikiri kwako huzidi kuzorota
Mara tu dalili zinapoanza, zitaendelea kuzorota na hatimaye kusababisha kifo katika miaka 13 hadi 15
Kipimo cha damu kinaweza kuwaambia madaktari ikiwa una jeni inayohusishwa na ugonjwa huo
Ni nini husababisha ugonjwa wa Huntington?
Ugonjwa wa Huntington husababishwa na jeni inayorithiwa kutoka kwa mmoja wa wazazi wako. Jeni hiyo husababisha kuharibika polepole kwa sehemu ya ubongo wako ambayo hukusaidia kufanya mwendo ambao ni laini na iliyoratibiwa
Dalili za ugonjwa wa Huntington ni zipi?
Dalili kwa kawaida huanza kwa umri wa utu uzima.
Dalili za kwanza za kawaida ni pamoja na:
Mwendo usiokusudiwa katika miguu na mikono yako
Kukopesa macho mara kwa mara
Kutembea kwa mkutuo
Mabadiliko ya kiakili na ya kitabia, kama vile kuchanganyikiwa, kukosa udhibiti wa uamuzi, unyogovu, au hasira
Ugonjwa unavyozidi kuwa mbaya, unaweza:
Kupoteza kumbukumbu na uwezo wako wa kufikiri vizuri (kupoteza kumbukumbu)
Kupata matatizo katika kufanya kazi za kimsingi kama vile kuvaa, kuoga, na kutumia choo
Hatimaye utahitaji matunzo ya wakati wote. Watu wengi hufariki miaka 13 hadi 15 baada ya dalili kuanza.
Madaktari wanawezaje kujua kama nina ugonjwa wa Huntington?
Ikiwa una dalili za ugonjwa wa Huntington, madaktari watafanya haya:
Vipimo vya kijeni kwenye damu yako
Kuhakikisha kuwa huna ugonjwa mwingine wa ubongo kwa kufanya vipimo kama vile tomografia ya kompyuta (uchanganuzi wa CT) au upigaji picha kwa mvumo wa sumaku (MRI)
Ikiwa vipimo vitaonyesha uwepo wa ugonjwa wa Huntington au ikiwa mtu katika familia yako alikuwa na ugonjwa wa Huntington, madaktari watapendekeza:
Ushauri nasaha kuhusu jeni
Ikiwa una ugonjwa wa Huntington, ushauri nasaha kuhusu jeni utakusaidia kuelewa hatari za kurithisha watoto wako ugonjwa huo.
Iwapo hujagunduliwa kuwa na ugonjwa wa Huntington lakini una historia ya ugonjwa huo katika familia, ushauri nasaha wa jeni unaweza kukusaidia kuamua kama ungependa kupimwa. Watu wengine hawataki kujua kama wana ugonjwa mbaya. Wengine wanataka kujua ikiwa watoto wao wowote wanaweza kuwa hatarini.
Madaktari hutibu vipi ugonjwa wa Huntington?
Hakuna tiba, lakini madaktari wanaweza kutibu dalili zako nyingi na kukusaidia kupanga maisha yako ya baadaye. Wanaweza kupendekeza:
Dawa ya kusaidia kutuliza dalili zako
Dawamfadhaiko, ikiwa una mfadhaiko
Unapaswa kuzungumza na daktari wako kuhusu maelekezo ya mapema. Katika maelekezo ya mapema, unaweka wazi chaguo zako za matibabu kwa kumwandikia daktari na familia yako wakati bado unaweza.