Distonia ni nini?

Distonia ni ugonjwa unaosababisha misuli yako kukaza yenyewe.

Mikazo hii ya misuli isiyo ya kawaida kutokana na distonia husababisha kukakamaa kwa misuli. Kukakamaa ni mkazo wa ghafla wa misuli (mshtuko) ambao huwezi kudhibiti. Mikakamao ya misuli yanaweza kutokea zaidi na zaidi baada ya muda na kuulazimisha mwili wako kuwa katika mkao usio wa kawaida au wa kupinda.

  • Mwanzoni, mishtuko wa misuli hutokea na kutoweka, kwa hivyo unaweza kupepesa macho yako, kusaga taya yako, kusogeza mikono yako, au kufanya harakati zingine.

  • Baadaye, misuli iliyoathiriwa inaweza kukaa katika mkazo huo na hivyo sehemu ya mwili wako kukwama

  • Distonia hutokea wakati kuna shughuli nyingi katika sehemu za ubongo zinazodhibiti misuli yako

  • Distonia inaweza kurithiwa au kusababishwa na matatizo ya ubongo au na dawa fulani

  • Madaktari hutibu sababu ya distonia na wanaweza kuagiza vidonge au sindano za kusaidia kulegeza misuli yako

Distonia husabaishwa na nini?

Distonia husababishwa na:

  • Shughuli nyingi zaidi katika sehemu za ubongo zinazodhibiti misuli yako

Uwepo wa shughuli nyingi zaidi, unaweza kutokea kwa sababu ya:

Dalili za distonia ni nini?

Dalili kuu ni:

  • Mkakamao wa misuli wa muda mrefu

Mwanzoni, mkakamao wa misuli hutokea mara moja tu kwa muda au inapowekewa mkazo. Baada ya muda, mkakamao wa misuli hutokea mara nyingi zaidi na kudumu kwa muda mrefu. Sehemu ya mwili ya iliyo na mkakamao inaweza kukwama katika mkao mmoja, wakati mwingine huwa na uchungu. Hii inaweza kusababisha ulemavu.

Distonia inaweza kutokea kwenye:

  • Kope, kwa kawaida huanza kama kupepesa macho zaidi, usumbufu kwenye macho, au kuathirika na mwanga mkali

  • Misuli ya shingo, na kusababisha kupinda kwa shingo, na uchungu ("shingo lililokakamaa").

  • Nyuzi za sauti, na kuathiri uwezo wako wa kuzungumza au ubora wa sauti yako

  • Misuli ya uso, ambayo inaweza kujumuisha kupepesa macho, kusaga taya bila kupenda, na sura za uso zisizo za kawaida.

  • Misuli yoyote unayotumia kupita kiasi—kwa mfano, vidole vya mpiga piano mtaalamu

Madaktari wanawezaje kujua iwapo nina distonia?

Madaktari hutambua distonia kulingana na dalili ulizo nazo na uchunguzi wa mwili. Hakuna vipimo maalum vya distonia, lakini madaktari wanaweza kuchunguza kama una tatizo la ubongo kwa kufanya haya:

Madaktari hutibu vipi tatizo la distonia?

Madaktari watatibu chanzo cha distonia ikiwa inawezekana. Matibabu mengine ni pamoja na:

  • Dawa, ikiwa ni pamoja na dawa za kuzuia neva na kutuliza kidogo (dawa ya kulegezaa mwili wako na kukusaidia kulala)

  • Sindano za dawa ya botulinum (Botox®) kwenye misuli iliyokazika, ambayo itailegeza

  • Matibabu ya kimwili

  • Wakati mwingine msisimko wa kina wa ubongo (elektrodi ndogo huwekwa kwenye ubongo wako ili kupunguza mkazo unaotokea mara kwa mara kwenye misuli)