Muhtasari wa Mfumo wa Neva

Imepitiwa/Imerekebishwa May 2024

Je, mfumo wa neva ni nini?

Mfumo wa neva ni mfumo wa kuchakata taarifa na mawasiliano ya mwili wako. Hupokea ujumbe, kuchakata taarifa, na kisha kutuma ishara kwa mwili wako wote kuuambia la kufanya.

Mfumo wa neva umeundwa na:

  • Ubongo

  • Uti wa mgongo

  • Neva

Mfumo wa neva unahusika katika kila kitu unachofikiri, kusema na kufanya.

  • Ubongo wako ni sawa na kituo cha msingi cha uchakataji (CPU) katika kompyuta

Ubongo hupokea habari kutoka kwenye macho, masikio, pua, ngozi na viungo vingine vya hisia. Huchakata taarifa na kuzalisha fikira na mawazo. Kisha ubongo hutuma ujumbe kwa mwili wako. Kwa mfano, huambia misuli yako jinsi ya kusogea ili uweze kutembea, kuzungumza, na kufanya mambo unayotaka mwili wako ufanye. Ubongo wako pia hudhibiti mambo mengi mwilini bila wewe kuyafikiria. Kwa mfano, ubongo wako hurekebisha kiotomatiki upumuaji wako, mapigo ya moyo na shinikizo la damu.

Uti wa mgongo huanzia kwenye ubongo na kushuka chini hadi kwenye mgongo wako ukipita kwenye uwazi wa kati wa mgongo wako. Neva katika ubongo huteremsha ujumbe kwenye uti wako wa mgongo. Kisha neva zingine kwenye uti wa mgongo wako hutuma ujumbe huo kwa mwili wako. Pia uti wa mgongo hubeba ujumbe kutoka kwenye mwili wako hadi kwenye ubongo wako.

  • Neva zako ni kama nyaya za ishara.

Kila neva ina nyuzi zitokazo kwenye seli nyingi za neva. Nyuzi hizo zimeunganishwa pamoja kwa ajili ya nguvu na ulinzi dhidi ya majeraha.

Mfumo mkuu wa neva ni ubongo na uti wa mgongo. Neva zilizo nje ya ubongo na uti wa mgongo zinaitwa mfumo wa neva wa pembezoni.

Je, mfumo wa neva hufanyaje kazi?

Mfumo wako wa neva umeunwa kwa:

  • Seli za neva na nyuzi zao

Kuna mabilioni na mabilioni ya seli za neva katika ubongo wako, uti wa mgongo wako, na mabonge yaliyo nje ya uti wa mgongo wako.

Kila seli ya neva ina kiini chake:

  • Kiini cha seli ya neva humeng'enya virutubishi na kudumisha seli

Kila seli ya neva ina nyuzi zinazoingia na kutoka ndani yake:

  • Nyuzi za kuingiza hupokea mawasiliano kutoka kwenye seli nyingine za neva au kutoka kwenye vipokezi katika viungo vyako vya hisia

  • Nyuzi hutuma mawimbi kwenye neva nyingine, kwenye misuli au viungo vingine

  • Mawimbi hufuata mkondo mmoja kwenye seli ya neva

Wakati mwingine nyuzi za neva zina urefu wa sentimita kadhaa. Kwa mfano, uzi mmoja wa neva unaweza kuanzia kwenye uti wa mgongo hadi kwenye kidole chako cha mguu. Baadhi ya nyuzi za neva zinazokwenda kwenye ngozi yako au viungo vyako zina vipokezi vya hisia. Kwa mfano, vipokezi vilivyo kwenye ncha ya nyuzi za neva kwenye ngozi yako hutambua vitu ambavyo vina makali au ni moto.

Seli za neva hutuma ishara zake kwa kutumia kemikali.

  • Kemikali hubadilika hatua kwa hatua kwenye uzi wa neva

  • Mabadiliko ya kemikali yanapofika kwenye ncha ya nyuzi za neva, hutoa kemikali nyingine zinazoitwa visafirisha ujumbe vya neva

  • Visafirisha ujumbe vya neva huteleza kwenye pengo la hadubini ambapo hugonga vipokezi vya kemikali vya seli nyingine

  • Visafirisha ujumbe vya neva huchochea mabadiliko ya kemikali katika seli ya pili

  • Ikiwa seli hiyo ni seli ya neva, basi mabadiliko ya kemikali yanafanyika kwenye nyuzi za seli hiyo ili kupitisha mawimbi

  • Wakati mwingine seli inayofuata si seli ya neva—kwa mfano, ikiwa seli inayofuata ni seli ya msuli, basi kisafirisha ujumbe au ishara cha neva husababisha mabadiliko ya kikemikali ambayo hufanya seli ya msuli kukaza

Muundo wa Kawaida wa Seli ya Neva

Seli ya neva (nyuroni) hujumuisha kiini kikubwa cha seli na nyuzi za neva— nyongeza moja iliyorefushwa (aksoni) kwa ajili ya kutuma vichocheo na kwa kawaida matawi mengi (dendraitisi) ya kupokea vichocheo. Vichocheo kutoka kwenye aksoni huvuka sinapsi (muungano uliopo baina ya seli 2 za neva) hadi kwa dendraiti ya seli nyingine.

Kila aksoni kubwa imezungukwa na oligodendrosaiti katika ubongo na uti wa mgongo na Seli za Schwann katika mfumo wa neva wa pembezoni. Utando wa seli hizi una mafuta (lipoprotini) yanayoitwa myelini. Utando umefungwa kwa kukaza kuzunguka aksoni, na kuunda ala yenye matabaka mengi. kifunika myelini kinafanana na mfuniko wa mpira, sawa na ule unaozunguka waya wa umeme. Vichocheo vya neva husafiri kwa haraka zaidi kwenye neva zenye vifunika myelini kuliko kwenye zile ambazo hazina.

Seli moja ya neva hutuma aina moja tu ya ishara ambayo haiwezi kubeba habari nyingi. Hata hivyo, mabilioni ya seli za neva zinapounganishwa sawa na ilivyo kwenye ubongo wako, hufanyika kichakataji taarifa chenye uwezo mkubwa.

Je, mfumo wa neva unaweza kupatwa na matatizo gani?

Matatizo mengi yanaweza kuathiri mfumo wa neva, ikijumuisha:

Mara baada ya kufa kwa seli za neva katika ubongo au uti wa mgongo wako, haziwezi kukua tena. Hata hivyo, wakati mwingine seli nyingine za ubongo zilizo karibu zinaweza kujifunza kuchukua nafasi ya seli za ubongo zilizokufa. Wakati mwignine nyuzi za neva zinaweza kukua tena ikiwa kiini cha seli zake hakijaharibika. Inaweza kuchukua miezi hadi nyuzi za neva kukua tena. Madaktari wakati mwingine wanaweza kuunganisha neva ndogo tena na kuzichochea zifanye kazi tena. Madaktari hawawezi kurekebisha uti wa mgongo au ubongo.

Je, ni kwa jinsi gani umri huathiri mfumo wa neva?

Watu wanapozeeka, huwa wanakuwa na seli za neva chache katika ubongo wao. Ikilinganishwa na vijana, wazee wana uwezekano mkubwa wa kuwa na:

  • Shida ya kukumbuka matukio ya hivi karibuni au kujifunza mambo mapya

  • Shida ya kutumia maneno

  • Mwitikio wao kuchukua muda mrefu

  • Kupungua kwa hisia katika ngozi zao

  • Kukosa ustadi

  • Kutekeleza polepole

Yafuatayo yanaweza kusaidia kuweka ubongo wako katika hali bora kwa muda mrefu: