Je, ubongo ni nini?

  • Ubongo wako ni sawa na kituo cha msingi cha uchakataji katika kompyuta

Ubongo hupokea habari kutoka kwenye macho, masikio, pua, ngozi na viungo vingine vya hisia. Huchakata taarifa, huzalisha fikira na mawazo, na kutuma ujumbe kwa mwili wako. Kwa mfano, huambia misuli yako jinsi ya kusogea ili uweze kutembea, kuzungumza, na kufanya mambo unayotaka mwili wako ufanye. Ubongo wako pia hudhibiti mambo mengi mwilini bila wewe kuyafikiria. Kwa mfano, ubongo wako hurekebisha kiotomatiki upumuaji wako, mapigo ya moyo na shinikizo la damu.

  • Unahitaji ubongo wako kuweza kutembea, kuzungumza, kuonja, kunusa, kusikia na kuona

  • Ubongo unahitaji kiasi kikubwa cha damu na oksijeni ili kufanya kazi—wakati wote, karibu 20% ya damu inayosukumwa na moyo wako huenda kwenye ubongo

Utazimia ikiwa mtiririko wa damu kwenye ubongo wako utasimama kwa zaidi ya sekunde 10.

Kuangazia Ubongo

Ubongo unajumuisha ubongombele, shina la ubongo na ubongonyuma. Kila nusu upande (nusu) wa ubongombele umegawanyika katika ndewe.

Je, zipi ni sehemu za ubongo?

Ubongo umekaa katika fuvu lako ukizungukwa na majimaji ambayo yanaulinda na kuushikilia. Majimaji haya yanaitwa majimaji ya ubongo na uti wa mgongo. Yanashikiliwa katika ubongo wako ndani ya tabaka 3 za utando unaoitwa meninji.

Ubongo una sehemu kuu 3:

  • Ubongombele: Sehemu kuu ya juu ya ubongo imegawanyika katika vipande vinavyoitwa ndewe—ndewe hizi hudhibiti fikra, mwendo, kuongea, kumbukumbu, mihemko, na hisia zako zote

  • Shina la Ubongo: Hii ni sehemu ya chini ya ubongo wako ambayo huungana na uti wa mgongo—shina la ubongo hudhibiti shughuli muhimu za mwili, kama vile fahamu, kupumua, shinikizo la damu, na mapigo ya moyo

  • Ubongonyuma: Sehemu ya ubongo wako iliyojitenga juu ya shina la ubongo wako ambayo inadhibiti usawa na uratibu

Ubongombele wako umegawanywa katika vipande viwili, kimoja upande wa kushoto na kingine upande wa kulia. Nusu ya upande wa kushoto hudhibiti upande wa kulia wa mwili wako na kinyume chake. Na hii ndio sababu pale mtu anapokuwa na kiharusi cha upande wa kushoto wa ubongo wake, hawezi kusogeza viungo vya upande wa kulia wa mwili wake.

Tishu Zinazofunika Ubongo

Kwenye fuvu la kichwa, ubongo umefunikwa na safu 3 za tishu zinazoitwa tando.

Je, ubongo hufanyaje kazi?

Ubongo wako umeundwa kwa:

  • Seli za neva na nyuzi zao

Kuna mabilioni na mabilioni ya seli za neva katika ubongo wako.

Kila seli ya neva ina kiini cha seli kidogo sana:

  • Kiini cha seli ya neva humeng'enya virutubishi na kudumisha seli

Kila kiini cha seli ya neva kina nyuzi zinazoingia na kutoka:

  • Nyuzi za kuingiza hupokea mawasiliano kutoka kwenye seli nyingine za neva au kutoka kwenye vipokezi katika viungo vyako vya hisia

  • Nyuzi za kutoa ishara hutuma ishara kwa neva zingine kwenye ubongo wako au uti wako wa mgongo

  • Mawimbi hufuata mkondo mmoja kwenye seli ya neva

Seli za neva hutuma ishara zao kwa kutumia kemikali.

  • Kemikali hubadilika hatua kwa hatua kwenye uzi wa neva

  • Mabadiliko ya kemikali yanapofika kwenye ncha ya nyuzi za neva, hutoa kemikali nyingine zinazoitwa visafirisha ujumbe vya neva

  • Visafirisha ujumbe vya neva huteleza kwenye pengo la hadubini ambapo hugonga vipokezi vya kemikali vya seli nyingine

  • Visafirisha ujumbe vya neva huchochea mabadiliko ya kemikali katika seli ya pili

  • Ikiwa seli hiyo ni seli ya neva, basi mabadiliko ya kemikali yanafanyika kwenye nyuzi za seli hiyo ili kupitisha mawimbi

Seli moja ya neva hutuma aina moja tu ya ishara ambayo haiwezi kubeba taarifa nyingi. Hata hivyo, mabilioni ya seli za neva zinapounganishwa sawa na ilivyo kwenye ubongo wako, hufanyika kichakataji taarifa chenye uwezo mkubwa.

Je, ubongo unaweza kupata matatizo gani?

Kuna matatizo mengi yanayoweza kuathiri ubongo wako, ikiwa ni pamoja na

Mara baada ya seli za neva zilizo katika ubongo wako kufa, haziwezi kuota tena. Hata hivyo, wakati mwingine seli nyingine za ubongo zilizo karibu zinaweza kujifunza kuchukua nafasi ya seli za ubongo zilizokufa. Ndiyo maana watu ambao wamepata kiharusi wakati mwingine hupata tena uwezo wao wa kusogeza viungo au kuzungumza. Inaweza kuchukua miezi kupata nafuu.