Je, neva ni nini?

Neva ni fungu la nyuzi za neva kutoka kwa seli nyingi za neva. Nyuzi hizo zimeunganishwa pamoja kwa ajili ya nguvu na ulinzi dhidi ya majeraha.

  • Neva zako ni kama nyaya za ishara

  • Neva hupeleka na kurudisha ujumbe kati ya ubongo au uti wa mgongo na mwili wako

  • Ujumbe kutoka kwenye ubongo hueleza mwili wako cha kufanya

  • Ujumbe kutoka kwenye mwili hueleza ubongo wako kile kinachoendelea kwenye mwili wako

  • Pale neva katika sehemu fulani ya mwili wako zinapoharibiwa au kushindwa kufanya kazi unaweza usiweze kusogeza au kuhisi sehemu ya mwili wako

Je, neva hufanyaje kazi?

Kuna mabilioni na mabilioni ya seli za neva katika ubongo wako, uti wa mgongo wako, na katika vikundi nje tu ya uti wa mgongo wako.

Kila seli ya neva ina kiini chake:

  • Kiini cha seli ya neva humeng'enya virutubishi na kudumisha seli

Kila kiini cha seli ya neva kina nyuzi zinazoingia na kutoka:

  • Nyuzi za kuingiza hupokea mawasiliano kutoka kwenye seli nyingine za neva au kutoka kwenye vipokezi katika viungo vyako vya hisia

  • Nyuzi hutuma mawimbi kwenye neva nyingine, kwenye misuli au viungo vingine

  • Mawimbi hufuata mkondo mmoja kwenye seli ya neva

Wakati mwingine nyuzi za neva zina urefu wa sentimita kadhaa. Kwa mfano, uzi mmoja wa neva unaweza kuanzia kwenye uti wa mgongo hadi kwenye kidole chako cha mguu. Baadhi ya nyuzi za neva zinazokwenda kwenye ngozi yako au viungo vyako zina vipokezi vya hisia. Kwa mfano, vipokezi vilivyo kwenye ncha ya nyuzi za neva kwenye ngozi yako hutambua vitu ambavyo vina makali au ni moto.

Kwa sababu kila nyuzi ya neva ni ndogo sana, nyuzi zimefungwa pamoja ili ziwe imara. Nyuzi kubwa hutoka kwenye uti wa mgongo wako na kugawanyika sawa na matawi ya mti ili kusambaa katika sehemu mbalimbali za mwili wako. Neva mbalimbali hupeleka na kurudisha ishara kwa sehemu mahususi ya mwili wako.

Seli za neva hutuma ishara zao kwa kutumia kemikali.

  • Kemikali hubadilika hatua kwa hatua kwenye uzi wa neva

  • Mabadiliko hayo ni ya haraka lakini sio ya haraka kama umeme

  • Mabadiliko ya kemikali yanapofika kwenye ncha ya nyuzi za neva, hutoa kemikali nyingine zinazoitwa visafirisha ujumbe vya neva

  • Visafirisha ujumbe vya neva huteleza kwenye pengo la hadubini ambapo hugonga vipokezi vya kemikali vya seli nyingine

  • Visafirisha ujumbe vya neva huchochea mabadiliko ya kemikali katika seli ya pili

  • Ikiwa seli hiyo ni seli ya neva, basi mabadiliko ya kemikali yanafanyika kwenye nyuzi za seli hiyo ili kupitisha mawimbi

Ili kusaidia ishara za kemikai kusafiri haraka, nyuzi za neva zimefunikwa kwa tabaka la mafuta linaloitwa kifunika myelini. Iwapo kifunika myelini kitaharibiwa, ujumbe ama haupitishwi au hupitishwa polepole kwenye neva.

Insulating a Nerve Fiber

Most nerve fibers inside and outside the brain are wrapped with many layers of tissue composed of a fat (lipoprotein) called myelin. These layers form the myelin sheath. Much like the insulation around an electrical wire, the myelin sheath enables nerve signals (electrical impulses) to be conducted along the nerve fiber with speed and accuracy. When the myelin sheath is damaged (called demyelination), nerves do not conduct electrical impulses normally.

Je, neva zinaweza kukumbana na matatizo gani?

Kuna matatizo mengi yanayoweza kuathiri neva:

Mara baada ya seli za neva kufa, haziwezi kuota tena. Hata hivyo, ikiwa kiini cha seli ya neva hakikudhurika, wakati mwingine nyuzi za neva zinaweza kuota tena pole pole. Madaktari wakati mwingine wanaweza kuunganisha neva zilizokatika na kuzifanya zifanye kazi tena. Kwa kawaida uharibifu wa kifunika myelini ni wa kudumu.