Paiodema gangrenosam ni nini?
Paiodema gangrenosam ni ugonjwa wa ngozi ambapo unapata majeraha makubwa kwenye ngozi yako, hasa kwenye miguu.
Huwapata hasa watu wenye umri kuanzia miaka 25 hadi 55
Madaktari hawajui chanzo chake ni nini, lakini mara nyingi huwapata watu ambao wana matatizo mengine ya kiafya, kama vile ugonjwa wa uchochezi wa matumbo
Wakati mwingine hutokea kwa ngozi iliyojeruhiwa hivi karibuni
Unapata viuvimbe au malengelenge madogo madogo ambayo hugeuka na kuwa vidonda vilivyo wazi
Matibabu yake hujumuisha kufunga vidonda, malai, na dawa
Je, nini husababisha paiodema gangrenosam?
Madaktari hawajui nini hasa husababisha paiodema gangrenosam, lakini wanadhani ni tatizo linalohusiana na mfumo wa kingamwili. Paiodema gangrenosam huwapata sana watu ambao wana matatizo fulani ya kiafya, kama vile:
Zipi ni dalili za paiodema gangrenosam?
Dalili za paiodema gangrenosam ni pamoja na:
Uvimbe au malengelenge mekundu ambayo hugeuka na kuwa jeraha lililo wazi, lenye uchungu ambalo hukua kwa haraka
Eneo lililoinuliwa kuzunguka jeraha ambalo ni jeusi au la zambarau
Homa
Hisia ya jumla ya kuumwa
Majeraha yatokanayo na paiodema gangrenosam yanaweza kuwa mabaya zaidi kutokana na:
Bayopsi (uondoaji wa kipande cha tishu kwa uchunguzi)
Kusafisha seli zilizokufa kutoka kwenye kidonda (inaitwa debridement)—japokuwa uondoaji wa seli zilizokufa husaidia kidonda kupona, kuondoa seli zilizokufa kwenye majeraha ya paiodema gangrenosam huyafanya yawe na hali mbaya zaidi badala ya kupata ahueni
Mara nyingine dalili zinaweza kusambaa katika maeneo mengine, kama vile eneo la tumboni, mifupa, mapafu, au misuli.
© Springer Science+Business Media
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina paiodema gangrenosam?
Mara nyingi madaktari wanaweza kufahamu ikiwa una paiodema gangrenosam kwa kutazama majeraha.
Je, madaktari hutibu vipi paiodema gangrenosam?
Madaktari hutibu paiodema gangrenosam kwa kutumia:
Kufunga vidonda ili kulinda ngozi yako
Kotikosteroidi
Mara nyingine dawa ya kutuliza mfumo wa kingamwili wako
Mara nyingi madaktari hawafanyi upasuaji, kwa sababu kufanya hivyo hufanya majeraha kuwa mabaya zaidi.