Ungonjwa wa Stevens-Johnson (SJS) na Toxic Epidermal Necrolysis (TEN)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Ugonjwa wa Stevens-Johnson (SJS) na ugonjwa wa kufa kwa seli za ngozi kutokana na sumu (TEN) ni nini?

Ugonjwa wa Stevens-Johnson (SJS) na ugonjwa wa kufa kwa seli za ngozi kutokana na sumu (TEN) ni aina ya ugonjwa uleule wa ngozi wa kutishia maisha. SJS inahusisha mwili wako kwa kiasi kidogo, na TEN inahusisha mwili wako kwa kiasi kikubwa. Yote husababisha upele, ngozi kubanduka, na majeraha.

  • SJS na TEN mara nyingi husababishwa na athari za dawa

  • Dalili za magonjwa haya mawili hujumuisha ngozi kubanduka, homa, maumivu ya mwili, upele mwekundu vilivyo bapa, na malengelenge na majeraha kwenye mdomo, macho, na uke wako

  • Matibabu hutolewa hospitalini katika kitengo cha wagonjwa mahututi na hujumuisha kiowevu, dawa, na kusitisha matumizi ya dawa yoyote ambayo inaweza kuwa imesababisha ugonjwa huo

Je, nini husababisha SJS na TEN?

SJS na TEN mara nyingi husababishwa na:

  • Athari za dawa, mara nyingi salfa na dawa za kuua bakteria au dawa za mshtuko (anticonvulsants)

Ni mara chache, matukio haya kusababishwa na maambukizi ya bakteria au chanjo.

SJS na TEN huwapata zaidi watu wenye:

Zipi ni dalili za SJS na TEN?

Dalili za SJS na TEN mara nyingi huanza wiki 1 hadi 3 baada ya kuanza kutumia dawa. Dalili za mwanzo hujumuisha:

  • Homa

  • Maumivu ya kichwa

  • Kikohozi

  • Macho mekundu, yaliyovimba

  • Maumivu ya mwili

Dalili za baadaye zinajumuisha:

  • Upele mwekundu, wenye umbo la bapa kwenye uso wako, shingo, na kiwiliwili, ambao husambaa katika maeneo mengine ya mwili

  • Malengelenge yanayojitokeza na kubanduka kwa urahisi

  • Malengelenge mdomoni, machoni na kwenye uke wako

Katika SJS, ngozi hubanduka katika maeneo madogo ya mwili wako. Katika TEN, maeneo ni makubwa na sehemu kubwa ya ngozi yako huathiriwa. Kadiri ngozi zaidi inavyobanduka, ndivyo hatari inavyoongezeka.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina SJS au TEN?

Madaktari wanaweza kufahamu kama una SJS au TEN kwa kukuuliza kuhusu dalili ulizonazo na kutazama ngozi yako. Pia wanaweza kuondoa kipande cha ngozi kwa uchunguzi (kuchukua kipande kidogo cha tishu ili kukichunguza kwenye hadubini).

Je, madaktari wanatibu vipi SJS na TEN?

Madaktari hukuhudumia hospitalini kwenye ICU (kitengo cha wagonjwa mahututi). Daktari atasitisha dawa yoyote ambayo inaweza kuwa imesababisha ugonjwa wako wa SJS au TEN.

Matibabu yanajumuisha:

  • Kiowevu kwa njia ya mshipa

  • Kubadilisha plazma (mchakato ambao huwaruhusu madaktari kuchuja baadhi ya vitu, kama vile dawa ambayo inasababisha athari uliyonayo, kutoka kwenye damu yako)

  • Globulini ya kingamaradhi

  • Wakati mwingine, dawa