Vipele vya Dawa

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Upele wa dawa ni nini?

Upele wa dawa ni mlipuko kwenye ngozi yako unaosababishwa na dawa.

  • Upele wa dawa kwa kawaida husababishwa na mmenyuko wa mzio kwa dawa unayotumia

  • Unaweza kupata upele wa dawa kutoka kwa dawa unayomeza, kuwekwa kwenye ngozi yako, au kupata kama sindano

  • Utapata upele au mabaka ya ngozi na kuwashwa, kuchubua, au maumivu

  • Ikiwa hujui ni dawa gani inayosababisha upele, daktari wako anaweza kukusitisha kutumia dawa zako zote kwa muda ili kujua

  • Upele wa dawa kawaida hupotea unapoacha kutumia dawa

  • Baadhi ya upele wa dawa ni mbaya vya kutosha kuhitaji matibabu

Je, nini husababisha upele wa dawa?

Upele wa dawa husababishwa na dawa unayotumia. Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha hili. Sababu za kawaida zaidi ni pamoja na:

  • Una mmenyuko wa mzio unaotokana na dawa—hii inaweza kutokea hata baada ya kuwa umetumia dawa hiyo kwa kipindi fulani

  • Dawa inafanya ngozi yako kudhurika zaidi kwa mwanga wa jua

Zipi ni dalili za upele utokanao na dawa?

Upele utokanao na dawa unaweza kuwa wa kawaida au mbaya. Unaweza kutokea ndani ya dakika chache tangu kutumia dawa au baada ya kutumia dawa kwa wiki kadhaa.

Dalili zinajumuisha:

  • Wekundu kiasi kwenye ngozi yako ulioambatana na uvimbe mdogo

  • Ngozi yako kubanduka kwa kiasi kikubwa

  • Maumivu au kuwasha/mwasho wa ngozi

  • Vidonda vya mdomo

Ikiwa una mmenyuko wa mzio wa dawa, unaweza kuwa na mabaka ya ngozi mbali na pua zinazotoa kamasi, macho yanayotoa machozi, na kuforota.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina upele unaosababishwa na dawa?

Madaktari watachunguza upele wako na kukuuliza kuhusu dawa zako zote za sasa ulizoandikiwa na daktari na zile zisizohitaji maagizo ya daktari. Watakuzuia kutumia dawa ambazo zina uwezekano mkubwa wa kuwa ndizo zilizosababisha upele ili kuona kama upele utatoweka. Mara nyingine, watafanya vipimo kwenye ngozi yako au kuondoa kipande cha tishu kwa uchunguzi (kuondoa kipande kidogo cha tishu ili kukichunguza kwenye hadubini).

Je, madaktari wanatibu vipi upele utokanao na dawa?

Madaktari wanatibu upele utokanao na dawa kwa:

  • Kusitisha dawa iliyousababisha—badala yake wanaweza kukuandikia dawa nyingine

  • Kwa kukufanya utumie malai ya antihistamini na kotikosteroidi ili kupunguza kuwasha/mwasho

  • Kukupatia dawa kupitia mshipa wako au kwa kukuchoma sindano, ikiwa una mmenyuko mkali wa mzio ambao umetokana na dawa hiyo