Je, mabaka ya ngozi ni nini?
Mabaka ya ngozi ni madoa yaliyoinuliwa, mekundu yanayowasha kwenye ngozi yako.
Mabaka ya ngozi kwa kawaida yanakuja na kuondoka kabisa, lakini wakati mwingine yanadumu kwa muda mrefu.
Mimenyuko ya mizio mara nyingi husababisha mabaka ya ngozi lakini kuna sababu nyinginezo
Nini kinachosababisha mabaka ya ngozi?
Mabaka ya ngozi kwa kawaida husababishwa na mmenyuko wa mzio wa:
Chakula
Kuumwa au kung'atwa na wadudu
Kemikali
Dawa
Mabaka kwenye ngozi yanaweza pia kusababishwa na:
Msongo wa mawazo na matatizo mengine ya kimihamko
Sababu za kimwili kama vile, shinikizo la damu, baridi, joto na mwanga
Magonjwa ya mfumo wa kinga kwenda kinyume na mwili (ugonjwa ambao unafanya mfumo wa kingamaradhi kushambulia tishu zake)
Wakati mwingine wewe na daktari wako hamtaweza kuelewa nini kilichosababisha mabaka ya ngozi yako.
Ni wakati gani ninapaswa kumwona daktari kuhusu mabaka ya ngozi yangu?
Ita gari la wagonjwa ikiwa ikiwa una mabaka ya ngozi na:
Unapata shida kupumua au kuforota (sauti ya mluzi unapopumua)
Koo lako lipo kama linafunga
Nenda kwenye kitengo cha dharura au kwa daktari mapema kadiri iwezekanavyo ikiwa una mabaka ya ngozi na:
Mabaka ya ngozi ni makali na yanazidi kuwa mabaya
Unaanza kujihisi mdhaifu na mwenye kizunguzungu
Una homa kali au mzizimo
Unarukaruka, una maumivi kwenye tumbo lako, au unaharisha (mara kwa mara, kinyesi laini au cha majimaji)
Mabaka ya ngozi yako ni meusi au yanageuka kuwa vidonda vya wazi
Mwone daktari ikiwa una:
Mabaka ya ngozi kwa sababu ya kuumwa na nyuki (kuzungumza na daktari wako kuhusu nini cha kufanya ikiwa utaumwa tena)
Mabaka ya ngozi yanayodumu kwa zaidi ya siku kadhaa
Mabaka ya ngozi pamoja na homa, kupungua uzani, vinundu vya limfu vilivyovimba, maumivu ya viungo, au kuvuja jasho usiku
Dalili za mabaka ya ngozi ni zipi?
Photo provided by Thomas Habif, MD.
Mabaka ya ngozi kwa kawaida:
Mabaka kwenye ngozi yako ambayo ni mekundu, yameinuka kidogo na yana mpaka unaoonekana dhahiri na katikati yanaweza kuwa dhahiri
Kwenye sehemu moja ya mwili wako au mwili mzima
Yanawasha sana
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina mabaka ya ngozi?
Daktari wako anaweza kujua kama una mabaka ya ngozi kwa kuangalia upele wako. Hata hivyo, wakati mwingine daktari atahitaji kufanya vipimo ili kujua kwa nini mabaka ya ngozi, hasa unapoendelea kuwa nayo tena na tena.
Madaktari wanatibu vipi mabaka ya ngozi?
Madaktari huenda wasihitaji kutibu mabaka ya ngozi ikiwa yataondoka yenyewe baada ya siku moja au mbili na yasirudi tena. Ikiwa kilichosababisha mabaka ya ngozi kinajulikana wazi, daktari wako atakushauri uepuke kitu hicho. Ili kupunguza dalili zako, daktari wako anaweza:
Akakuomba uoge kwenye maji ya baridi, si kujikuna ngozi yako na kuvaa nguo zisizobana hadi mabaka ya ngozi yaondoke
Atakupatia dawa fulani, kama vile antihistamini au vidonge vya kotikosteroidi ili kutibu mwasho, inategemeana na jinsi dalili zako zilivyo mbaya
Atakuomba uache kutumia dawa, ikiwa inawezekana, ili kuona endapo hiyo inasaidia
Vidonge vya antihistamini vinaweza kukufanya usinzie, haswa kwa wenye umri zaidi. Kuwa mwangalifu kuhusu kuzitumia ikiwa unahitaji kuendesha gari au kutumia zana za kielekroniki. Kwa upande mwingine, antihistamini inaweza kukusaidia kulala usiku.
Ninawezaje kuzuia mabaka ya ngozi?
Ikiwa wewe na daktari wako mtajua kile kilichosababisha mabaka ya ngozi, unaweza ukazuia mabaka ya ngozi kwa kuepuka kisababishi hicho. Lakini mabaka ya ngozi yakiwa yanaendelea kurudi na sababu haijulikani, unaweza kuhitaji kutumia dawa fulani kila siku ili kuzuia hali hii isitokee.