Ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana ni nini?
Ugonjwa wa ngozi ni istilahi ya jumla inayorejelea mwasho na uvimbaji wa kawaida wa ngozi.
Picha kwa hisani ya Thomas Habif, MD.
Ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana ni upele unaosababishwa na kugusa kitu ambacho kinasababisha mjibizo kwenye ngozi yako. Kitu hicho kinaweza kuwasha ngozi yako (ugonjwa wa mwasho wa ngozi unaosababishwa na kugusana au unaosababisha mmenyuko wa mzio) au kusababisha mmenyuko (ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na mzio wa kugusana).
Maelfu ya vitu vinaweza kusababisha ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana unaowasha au ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana wa mzio.
Ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana unaweza kuanza wakati wowote kwenye maisha yako
Ikiwa utapata ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana kutoa kwenye kitu fulani mara moja pengine utaupata kila wakati utakapogusa kitu hicho
Njia bora ya kutibu ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana ni kuepuka kitu chochote kinachousababisha
Ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana unaweza kuchukua wiki 3 kuondoka
Kugusa upele hakutaueneza kwa mtu mwingine
Nini kinachosababisha ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana?
Ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana unaowasha unasababishwa na vitu vinavyowasha ngozi yako unapovigusa, kama vile:
Kemikali, kama vile vifaa vya usafi vya kukaisha maji na vifaa vya kuondoa rangi ya kucha
Baadhi ya vipodozi, deodranti na sabuni
Pombe ya kusugulia
Viyeyushaji thabiti na blichi
Mimea fulani, kama vile poinsettias na pilipili
Wakati mwingine majimaji ya mwili, kama vile mkojo na mate
Watu wengine wanadhurika kwa urahisi sana na vitu vinavyowasha kuliko wengine.
Ugonjwa wa mzio wa ngozi unaosababishwa na kugusana ni wakati ambapo mfumo wako wa kingamwili unapata mmenyuko kutokana na kitu kilichogusa ngozi yako. Unaweza kuwa na mzio kutokana na vitu vingi mbalimbali, lakini sababu kubwa zaidi ya ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana wa mzio ni:
Mimea fulani, kama vile sumu mwefeu
Mpira, ikiwa ni pamoja na latex
Dawa za kuua bakteria na dawa nyinginezo zinawekwa kwenye ngozi
Manukato na marashi
Vihifadhi chakula
Baadhi ya metali kama vile nikeli na kobalti
Wakati mwingine unapata ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana mwanga wa jua unapowaka kwenye ngozi ambayo ina vitu fulani juu yake, kama vile:
Vizuia jua
Losheni ya kupaka baada ya kunyoa
Marashi fulani
Dawa fulani za kuua bakteria unazoweka kwenye ngozi yako
Lami ya makaa ya mawe
Mafuta
Mimea
Vinyunyizi fulani kama vile viua wadudu
Dalili za ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana ni zipi?
Dalili zinajumuisha:
Kuwashwa na wakati mwingine kuungua au maumivu
Vipele vyakundu, wakati mwingine ukiwa na uvimbe au malengelenge madogo
Ngozi kavu, yenye magamba au iliyopasuka ikiwa ulipata ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana muda mrefu uliopita
Wekundu zaidi, kutoka machozi na kuvimba ikiwa ngozi itaambukizwa
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kupitia kugusana?
Kwa kawaida madaktari wanaweza kufahamu kuwa una ugonjwa wa ngozi unaotokana na kugusana kwa kuangalia vipele vyako. Hata hivyo, inaweza kuwa vigumu kujua ni kitu gani hasa kilichosababisha mjibizo.
Ikiwa hujui sababu ya vipele vyako, daktari wako anaweza kufanya vipimo ili kujua nini kilichosababisha. Hizi zinaweza kujumuisha vipimo vya mzio. Katika vipimo vya mzio, daktari wako anaweka viwango vidogo vya vitu tofuati kwenye ngozi yako kuona ikiwa vinaweza kusababisha ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kugusana.
Madaktari wanatibu vipi ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kugusana?
Kwanza madaktari wanatibu ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kugusana kwa kuhakikisha hukutani zaidi na kitu ambacho kimesababisha upele. Mara kitu hicho kinapoondoka, upele hupotea wenyewe.
Mwasho na malengelenge yanaweza kupata unafuu kupitia:
Krimu ya kotikosteroidi
Vidonge vya antihistamini
Kuweka kitambaa kilicholowekwa kwenye maji baridi au aluminum acetate (mchanganyiko wa Burow) kwenye upele mara kadhaa kwa siku
Oga kwa maji baridi kwa kuongeza shayiri ya unga laini (bidhaa inayotengenezwa kwa unga laini wa shayiri)
Dawa ya kuua bakteria, ikiwa ngozi itaambukizwa
Kotikosteroidi ya kunywa na dawa ambazo zinapunguza kasi ya mfumo wa kingamaradhi ikiwa ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kugusana ni mkali
Vidonge vya antihistamini vinaweza kukufanya usinzie, haswa kwa wenye umri zaidi. Kuwa mwangalifu kuhusu kuzitumia ikiwa unahitaji kuendesha gari au kutumia zana za kielekroniki. Kwa upande mwingine, antihistamini inaweza kukusaidia kulala usiku.
Kuna krimu kadhaa za mwasho ambazo unaweza kununua bila kuandikiwa na daktari. Krimu za antihistamini na krimu za kufisha ngozi ganzi zilizo na benzokaini wakati mwingine husababisha madhara kwenye ngozi, hivyo madaktari hawapendelei uzitumie.
Ninawezaje kuzuia ugonjwa wa ngozi unaosababishwa na kugusana?
Epuka kugusana na vitu vinavyowasha ngozi yako au vinavyokusababishia mmenyuko wa mzio.
Ikiwa utagusana na kitu, osha ngozi yako kwa sabuni na maji baada tu ya kugusana. Ikiwa utalazimika kugusa kitu hicho, vaa glavu, nguo au krimu ya kizuizi inayozuia ngozi yako isiguswe.