Mwasho ni hisia isiyopendeza kwenye ngozi yako ambayo inafanya utake kujikuna.

  • Kuwashwa kunaweza kusababishwa na matatizo mengi mbalimbali ya ngozi

  • Mwasho unaweza pia kusababishwa na mmenyuko wa mzio au tatizo ambalo linaathiri mwili wako wote

  • Unaweza kuwashwa kwenye sehemu moja tu au mwili mzima kulingana na kisababishi

  • Kujikuna kunaweza kufanya mwasho uwe mbaya zaidi na kuharibu ngozi yako

  • Kuoga mara chache zaidi, kutumia losheni au krimu na kutumia kiongeza unyevu nyumbani au kazini kunaweza kusaidia mwasho upungue

  • Matibabu mengine yanategemea kisababishi

Ni nini husababisha mwasho?

Mwasho kwa kawaida unasababishwa na matatizo ya ngozi, kama vile:

  • Ngozi kavu, hasa kwa watu wenye umri mkubwa

  • Upele, kama vile eksema, wakati mwingine huitwa ugonjwa wa ngozi wa atopiki

  • Kuumwa na wadudu

  • Mmenyuko wa mzio kwenye vitu vinavyogusa ngozi, kama vile sumu ya mwefeu

  • Maambukizi ya ngozi yanayosababishwa na kuvu au vimelea

Wakati mwingine, mwasho husababishwa na matatizo ndani ya mwili wako, kama vile:

Ni wakati gani ninapaswa kumwona daktari kuhusu kuwashwa?

Nenda kwa daktari mara moja ikiwa una mwasho na yoyote kati ya ishara hizi za onyo:

  • Maumivu tumboni mwako

  • Ngozi na macho yako kuwa ya manjano

  • Kuhisi kiu sana, kukojoa sana na kupungua uzani

Ita ambyulensi au nenda kwenye kitengo cha dharura moja kwa moja ikiwa unapata shida kupumua au kuhisi kuzimia. Hiyo inaweza kumaanisha una mmenyuko mkali wa mzio.

Mwonde daktari ndani ya wiki moja hivi ikiwa una:

  • Mwasho mkali

  • Upele unaozidi kuwa na hali mbaya au unaosambaa

  • Mwasho na kupungua uzani, kuchoka sana, au kutoka jasho kitandani wakati wa usiku

Je, nitarajie nini ninapokwenda kumwona daktari wangu?

Madaktari watauliza kuhusu dalili zako na kuangalia kwenye ngozi yako. Mara nyingi, madaktari wanaweza kujua kinachosababisha mwasho wako bila kufanya vipimo.

Wakati mwingine madaktari wanaweza kufanya vipimo kama vile:

  • Ikiwa daktari hana uhakika, atachukua sampuli ya ngozi yako kuichunguza kwa kutumia hadubini (kukata kipande cha tishu kwa ajili ya uchunguzi).

  • Vipimo vya mzio

  • Vipimo kujua ikiwa una tatizo kwenye sehemu nyingine ya mwili wako ambayo inasababisha mwasho

Madaktari wanatibu vipi mwasho?

Madaktari wanatibu tatizo linalosababisha wewe kuwashwa. Madaktari wanaweza pia kukuambia:

  • Uepuke kitu chochote ambacho kinaweza kuwa kinasababisha mwasho au kufanya hali iwe mbaya zaidi

  • Usioge mara nyingi zaidi na utumie maji baridi badala ya moto

  • Utumie losheni au krimu za kulainisha ngozi

  • Kulainisha hewa nyumbani kwako au kazini

  • Usivae nguo zinazobana au za sufu

  • Utumie vidonge vya antihistamini (dawa zinazosaidia kupunguza mwasho)

Vidonge vya antihistamini vinaweza kukufanya usinzie, haswa kwa wenye umri zaidi. Kuwa mwangalifu kuhusu kuzitumia ikiwa unahitaji kuendesha gari au kutumia zana za kielekroniki. Kwa upande mwingine, antihistamini inaweza kukusaidia kulala usiku.

Unaweza kununua krimu za mwasho bila kuandikiwa na daktari. Lakini zungumza na daktari wako kabla hujazituia. Krimu za kotikosteroidi kama vile haidrokotisoni, zinaweza kusaidia aina fulani za mwasho lakini ni mbaya kwa wengine (kwa mfano, mwasho unaosababishwa na maambukizi ya ngozi). Krimu za antihistamini na krimu za kufisha ngozi ganzi zilizo na benzokaini wakati mwingine husababisha madhara kwenye ngozi, hivyo madaktari hawapendelei uzitumie.