Erithema Matifomu

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Erithema matifomu ni nini?

Erithema matifomu ni tatizo la ngozi linalosababisha madoa mekundu kwenye ngozi, na ngozi kuvimba.

  • Unapata madoa mekundu ambayo kwa ghafla hutokea kwenye viganja, nyayo, mikono, miguu na kwenye uso wako, na baadaye yanaweza kusambaa kwenye sehemu nyingine za mwili wako

  • Madoa haya mara nyingine hufanana na shabaha

  • Pia unaweza kupata vidonda vya mdomo

  • Mara nyingi utapata ahueni ndani ya wiki 2 hadi 4

  • Pia madaktari wanaweza kutumia dawa kuzuia kuwasha/mwasho

  • Ikiwa unapata erithema matifomu mara kwa mara, daktari wako anaweza kukuandikia dawa za kuzuia virusi

Je, ni nini husababisha erithema matifomu?

Erithema matifomu mara nyingi husababishwa na athari za:

Erithema matifomu husababishwa na maambukizi mengine au dawa au chanjo fulani mara chache.

Zipi ni dalili za erithema matifomu?

Dalili zinajumuisha:

  • Uvimbe mwekundu kwenye viganja, nyayo, mikono, miguu na usoni ambao hukua katika umbo la mviringo ambalo linaweza kufanana na shabaha

  • Madoa mekundu yenye pete zilizofifia ndani ya doa, na eneo la kati lenye rangi ya zambarau na malengelenge madogo madogo (majeraha ya "shabaha")

  • Mara nyingi, mwasho

  • Malengelenge au vidonda vyenye maumivu kwenye midomo yako na katika utando wa mdomo wako

Upele unaweza kuondoka wenyewe baada ya wiki kadhaa lakini unaweza kurejea kila mara.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina erithema matifomu?

Madaktari wanaweza kugundua kuwa una erithema matifomu kwa kutazama upele. Wanaweza kukutazama kwa umakini ili kuhakikisha kwamba si hali mbaya zaidi yenye kufanana na hiyo.

Je, madaktari wanatibu vipi erithema matifomu?

Erithema matifomu hupungua makali pasipo matibabu. Ikiwa dalili zako zinakupa wasiwasi, madaktari wanaweza kukutibu kwa kutumia:

  • Malai ya kuzuia kuwasha/mwasho

  • Dawa za ganzi kwa ajili ya malengelenge ya mdomo ikiwa yanasababisha matatizo ya kula na kunywa

  • Wakati mwingine, dawa za kuzuia virusi ikiwa unapata erithema matifomu kila mara, au ikiwa madaktari wanahisi hali yako ya erithema matifomu inasababishwa na herpesi