Haiba yako ni njia yako ya kipekee ya kufikiria, kuelewa, kuitikia, na kuhusiana na watu.
Matatizo ya utu sio tu kuwa na sifa zisizo za kawaida. Ni pale sifa zako zinasababisha matatizo makubwa kwako au ni kizingiti katika kuingiliana na watu wengine.
Ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi ni nini?
Ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi ni:
Mkondo wa kubadilika sana kwa hisia, uhusiano na tabia
Watu walio na ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi mara nyingi:
Hushikwa na hofu kubwa kwa ghafla au kukasirika wakati rafiki amechelewa kwa dakika chache au anaghairi miadi, ambayo huwafanya wahisi kutelekezwa
Wana hasira ya haraka na hupigia kelele marafiki, wapenzi na familia, haswa wakati wanafikiria kuwa mtu hafikii matakwa yao ya juu ya usaidizi
Hubadilisha maono yao kwa haraka, kama vile kutoka kusifu mtu hadi kwa ghafla kuanza kukosoa kwa sana
Kufanya vitu visivyo vya busara bila kufikiria, kama vile kushiriki ngono isiyo salama, kutumia pesa kupita kiasi, kuendesha gari bila kujali, kutumia dawa au kunywa pombe nyingi
Kujihujumu wenyewe wakati wako karibu kufikia lengo, kama vile kukataa kwenda shuleni mara tu kabla ya mahafali
Kujiumiza wenyewe kwa makusudi, kama vile kwa kujikata au kujichoma
Kuunda hali ya hatari, kama vile kujaribu kujitia kitanzi, ili kuzuia watu wengine kuwatelekeza
Ingawa mambo mengi ya kujidhuru wanayofanya si ya kufisha, karibu mtu 1 kati ya 10 walio na haiba ya mpaka wa kibinafsi hufariki kutokana na kujiua.
Hata kama wana uhitaji sana, watu walio na ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi kwa kawaida huwa na uhusiano usio thabiti. Wanaweza kuacha kwa ghafla kusifu rafiki na kuanza kukosoa na kuwaacha.
Ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi huwapata zaidi wanawake kuliko wanaume. Watu walio na ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi wanaweza pia kuwa na matatizo ya kula, wasiwasi, mfadhaikomsongo wa mawazo wa baada ya mshtuko (PTSD), au tatizo la matumizi ya pombe au dawa za kulevya.
Ni nini husababisha ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi?
Ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi una uwezekano mkubwa wa kusababishwa na haya mawili:
Jeni (maelezo ya jenetiki yanayopitishwa kwako kutoka kwa wazazi wako)—ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi huendelea kwenye familia
Mfadhaiko katika utotoni, kama vile dhuluma za kingono au kimwili, kutelekezwa au kuachanishwa na mzazi
Madaktari hutibu vipi ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi?
Madaktari hutibu ugonjwa wa haiba ya mpaka wa kibinafsi kwa:
Tiba (binafsi na kikundi)
Dawa ya hisia na wasiwasi