- Muhtasari wa Matatizo ya Haiba
- Ugonjwa wa Haiba ya Kupinga Jamii
- Ugonjwa wa Haiba ya Kuepuka Watu
- Ugonjwa wa Haiba ya Mpaka wa Kibinafsi:
- Ugonjwa wa Haiba ya Utegemezi
- Ugonjwa wa Haiba ya Kuigiza
- Haiba ya Kujihusudu
- Ugonjwa wa Haiba ya Kutojizuia Kurudiarudia Tendo
- Ugonjwa wa Haiba ya Wazimu wa Wasiwasi
- Ugonjwa wa Haiba ya Kujitenga
- Ugonjwa wa Haiba ya Kutopenda Ushirikiano
Haiba yako ni njia yako ya kipekee ya kufikiria, kuelewa, kuitikia, na kuhusiana na watu.
Matatizo ya utu sio tu kuwa na sifa zisizo za kawaida. Ni pale sifa zako zinasababisha matatizo makubwa kwako au ni kizingiti katika kuingiliana na watu wengine.
Ugonjwa wa haiba ya kutopenda ushirikiano ni nini?
Watu walio na ugonjwa wa haiba ya kutopenda ushirikiano:
Wana tabia isiyo ya kawaida, hawako sawa mahali kuna watu wengine na kuna vile hawazingatii ukweli
Watu walio na ugonjwa wa haiba ya kutopenda ushirikiano mara nyingi:
Huepuka hali za kijamii na kuchagua kuwa peke yao
Hawana marafiki wa karibu
Wana tatizo kuelewa hisia za watu wengine
Hufikiria kwa njia za ajabu, zisizo za kawaida, kama vile kuamini kuwa wanaweza kudhibiti mtu kwa kutumia akili yao
Wanashuku na kutoamini, kama vile kuamini kimakosa kuwa mtu anataka kuwaumiza
Hutumia maneno kwa njia zisizo za kawaida, kwa hivyo matamshi yao ni ya ajabu
Wanavalia isivyo kawaida, kama vile kuvalia mavazi chafu au yenye ukubwa usiowafaa
Pia wanaweza kuwa na mfadhaiko, au tatizo la matumizi ya pombe au dawa za kulevya.
Ugonjwa wa haiba ya kutopenda ushirikiano unafanana na lakini si mkali kama skizofrenia, ambayo husababisha mawazo na tabia mbaya zaidi na za ajabu.
Ni nini husababisha ugonjwa wa haiba ya kutopenda ushirikiano?
Kuna uwezekano mkubwa kuwa inasababishwa na jeni zako. Ni ya kawaida zaidi kwa watu ambao wana wanafamilia walio na skizofrenia.
Je, madaktari wanatibu vipi ugonjwa wa kutopenda ushirikiano?
Madaktari wanatibu ugonjwa wa kutopenda ushirikiano kwa:
Dawa (dawa ya skizofrenia na dawa za kuzuia msongo wa mawazo)
Tiba