- Muhtasari wa Matatizo ya Haiba
- Ugonjwa wa Haiba ya Kupinga Jamii
- Ugonjwa wa Haiba ya Kuepuka Watu
- Ugonjwa wa Haiba ya Mpaka wa Kibinafsi:
- Ugonjwa wa Haiba ya Utegemezi
- Ugonjwa wa Haiba ya Kuigiza
- Haiba ya Kujihusudu
- Ugonjwa wa Haiba ya Kutojizuia Kurudiarudia Tendo
- Ugonjwa wa Haiba ya Wazimu wa Wasiwasi
- Ugonjwa wa Haiba ya Kujitenga
- Ugonjwa wa Haiba ya Kutopenda Ushirikiano
Haiba yako ni njia yako ya kipekee ya kufikiria, kuelewa, kuitikia, na kuhusiana na watu.
Matatizo ya utu sio tu kuwa na sifa zisizo za kawaida. Ni wakati tabia za haiba zinasababisha matatizo makubwa kwenye maisha yako au kukuzuia kushirikiana kawaida na wengine.
Ugonjwa wa Haiba ya kuepuka watu ni nini?
Ugonjwa wa haiba ya kuepuka watu ni:
Mtindo wa kuepuka watu na hali za kijamii kwa kuogopa kukataliwa au kukosolewa
Watu walio na ugonjwa wa haiba ya kuepuka watu:
Hawajithamini na wanahisia mbaya wakikosolewa
Wanataka marafiki lakini wana tatizo kutengeneza urafiki
Huepuka hali za kijamii kwa sababu wana fedheha au kuogopa au kuchekelewa
Huepuka kuingiliana na watu wageni au kuchukua jukumu mpya kazini
Kwa sana hunyamaza na kuwa na aibu kwa sababu wanaogopa kuwa watasema jambo lisilofaa
Hujiona kuwa hawastahili na kuchukulia kuwa watu wengine hawawathamini
Hawataki kujaribu shughuli mpya au kuchukua hatari
Watu wengi wana wasiwasi kidogo katika hali za kijamii au wakati wanapatana na watu wageni. N hakuna mtu hufurahia kukosolewa. Lakini aina hizi za hisia zinaweza kuwa tatizo zikizuia watu kufaulu kazini au kufurahia maisha ya kawaida au ikiwa watu wanajawa sana na ugumu wao.
Ugonjwa wa haiba ya kuepuka watu unatokea sana kwa wanawake. Watu walio na tatizo hili mara nyingi wana msongo wa mawazo, Tatizo la kutojizuia kurudiarudia tendo (OCD) , wasiwasi, au tatizo lingine la haiba.
Ni nini husababisha ugonjwa wa haiba ya kuepuka watu?
Ugonjwa wa haiba ya kuepuka watu una uwezekano mkubwa wa kusababishwa na haya mawili:
Jeni zako (chembe za urithi kutoka kwa wazazi wako)
Uliyopitia na makuzi
Madaktari hutibu vipi ugonjwa wa haiba ya kuepuka watu?
Madaktari hutibu ugonjwa wa haiba ya kuepuka watu kwa kutumia:
Ushauri nasaha au tiba ya mazungumzo ambayo huangazia ustadi wa kijamii
Wakati mwingine, aina zingine za tiba
Dawa kwa wasiwasi na msongo wa mawazo wowote