Haiba yako ni njia yako ya kipekee ya kufikiria, kuelewa, kuitikia, na kuhusiana na watu.
Matatizo ya utu sio tu kuwa na sifa zisizo za kawaida. Ni pale sifa zako zinasababisha matatizo makubwa kwako au ni kizingiti katika kuingiliana na watu wengine.
Haiba ya kujihusudu ni nini?
Haiba ya kujihusudu ni:
Mkondo wa kuhisi kuwa juu ya watu wengine, kuhitaji kupendwa na kukosa uweze wa kuhisi maono ya wengine
Watu walio na haiba ya kujihusudu mara nyingi:
Kufikiria ni wa maana sana na maalum kuliko watu wengine
Kutia chumvi mafanikio yao wenyewe na kudharau watu wengine
Wana hisia mbaya kwa kufeli au kukosolewa kwa aina yoyote, ambayo huwafanya wenye hasira na wenye msongo wa mawazo
Kuwaza kuhusu kuwa mahiri, warembo au muhimu sana
Kutumia wengine vibaya
Wanahitaji kusifiwa sana na watu kuwategemea
Anawaonea wengine wivu na mara nyingi hudhania kuwa wengine wanawaonea wivu
Watu walio na haiba ya kujihusudu wana uwezekano mkubwa wa kuwa wanaume. Pia wanaweza kuwa na msongo wa mawazo, anoreksia, matatizo ya pombe au dawa, na matatizo mengine ya haiba.
Watu wengi wanajivunia mafanikio yao. Na karibu kila mtu anapenda kuwasifu na hawapendi kukosolewa. Hata hivyo, aina hizi za tabia hukuwa tatizo wakati watu wanakasirika au kusikitika bila kusifiwa wakati wote au wakati kutoweza kwao kukubali kukosolewa na hitaji lao la kudharau wengine linasababisha matatizo kazini au kwenye uhusiano.
Ni nini husababisha ugonjwa wa haiba ya kujihusudu?
Ugonjwa wa haiba ya kujihusudu una uwezekano mkubwa wa kusababishwa na haya mawili:
Jeni zako (chembe za urithi kutoka kwa wazazi wako)
Hali na malezi yako, kama vile jinsi wazazi wako walivyokutendea
Madaktari hutibu vipi ugonjwa wa haiba ya kujihusudu?
Madaktari hutibu ugonjwa wa haiba ya kujihusudu kwa:
Tiba