Haiba yako ni njia yako ya kipekee ya kufikiria, kuelewa, kuitikia, na kuhusiana na watu.
Matatizo ya utu sio tu kuwa na sifa zisizo za kawaida. Ni pale sifa zako zinasababisha matatizo makubwa kwako au ni kizingiti katika kuingiliana na watu wengine.
Ugonjwa wa haiba ya kuigiza ni nini?
Ugonjwa wa haiba ya kuigiza ni:
Mkondo wa kutaka kuwa kiangaziwa na kujibeba kwa njia za maigizo, zisizo mwafaka ili kuangaziwa
Ugonjwa wa haiba ya kuigiza huwapata zaidi wanawake. Mara nyingi watu:
Wamechangamka, wana shauku, wacheshi na haiba
Wanataka kuangaziwa na wana msongo wa mawazo wakati hawaangaziwi
Huvalia nguo za kuvutia au za juu zisizofaa kazini au shuleni ili kupata mvuti
Wana hisia zinazobadilika haraka zaidi ambazo wanaonyesha kwa njia ya maigizo
Wanashawishika kwa urahisi na wengine
Wana tatizo la kuingiliana sana
Wanataka mambo mapya na msisimko na wanachoshwa kwa urahisi kwa hivyo wanaweza kubadilisha kazi sana na kubadilisha marafiki wao
Watu wengi wana haiba na ucheshi na wanapenda kuangaziwa. Lakini aina hii ya tabia inaweza kuwa tatizo ikiwa watu lazima wawe viangaziwa na kuwa na msongo wa mawazo wakati hawaangaziwi. Ni tatizo pia ikiwa watu hawawezi kudumisha uhusiano au kazi kwa sababu ya hitaji lao la maigizo na mabadiliko mengi.
Watu walio na ugonjwa wa haiba ya kuigiza wanaweza pia kuwa na matatizo mengine ya haiba au msongo wa mawazo.
Ugonjwa wa haiba ya kuigiza husababishwa na nini?
Ugonjwa wa haiba ya kuigiza una uwezekano mkubwa wa kusababishwa na haya mawili:
Jeni zako (chembe za urithi kutoka kwa wazazi wako)
Hali na malezi yako, kama vile jinsi wazazi wako walivyokutendea
Madaktari hutibu vipi ugonjwa wa haiba ya kuigiza?
Madaktari hutibu ugonjwa wa haiba ya kuigiza kwa:
Tiba