Sumu ya Hidrokaboni

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2023

Hidrokaboni ni kemikali zilizo kwenye gundi, petroli, rangi na kiowevu cha kulainisha rangi ili iwe rahisi kupaka, na mafuta ya taa.

Je, sumu ya hidrokaboni ni nini?

Sumu ya hidrokaboni ni maradhi yanayotokana na kumeza au kupumua mvuke kutoka kwa bidhaa za hidrokaboni.

  • Watoto wengi wadogo wanaomeza bidhaa hizi na kuathiriwa na sumu watapona

  • Vijana na watu wazima wanaovuta mvuke kwa madhumuni ya kulewa (inayojulikana kama kuvuta, kunusa au kunusa kwa kutumia mfuko) wanaweza kufa kwa mshtuko wa moyo (wakati mioyo yao itakaposita kupiga) au ubongo kuharibika

  • Kumeza hidrokaboni kunaweza kusababisha kuwashwa na kisha maambukizi kwenye mapafu

  • Athari kali ya sumu huathiri ubongo, moyo, uboho na figo

Ikiwa unafikiri wewe au mtu mwingine anaweza kuwa na sumu, piga simu kwa usaidizi wa dharura wa matibabu (911 katika maeneo mengi nchini Marekani) mara moja.

Je, dalili za athari ya sumu ya hidrokaboni ni zipi?

  • Kukohoa

  • Kukabwa koo

  • Kupumua haraka

  • Hisia ya kuchomwa ndani ya tumbo

  • Ngozi ya bluu (kwa sababu ya viwango vya chini vya oksijeni katika damu)

  • Kupatwa na usingizi kila mara

  • Matatizo ya kupumua—inaweza kuchukua saa kadhaa hili kutokea

  • Kutekeleza mambo ovyo (kuchanganyikiwa)

  • Vifafa (Pale ambapo mwili wako husogea au kutetemeka bila udhibiti wako)

  • Koma (unapopoteza fahamu na kushindwa kuamka)

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina sumu ya hidrokaboni?

Madaktari watashuku athari ya sumu ya hidrokaboni kulingana na dalili zako na maelezo ya kile kilichotokea. Wanaweza kunusa hidrokaboni au kuona alama za rangi au mafuta kwenye mwili wako au nguo.

Madaktari watafanya:

  • Watafanya eksirei ya kifua ili kuangalia kama kuna majimaji kwenye mapafu yako

  • Watapima kiwango cha oksijeni katika damu yako

  • Watafanya uchunguzi wa MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku) ikiwa wanahitaji kuchunguza uharibifu wa ubongo

Je, madaktari hutibu aje athari ya sumu ya hidrokaboni?

Madaktari watafanya:

  • Je, umevua nguo zozote zilizogusa hidrokaboni?

  • Osha ngozi yako vizuri

  • Watukupa oksijeni au, ikiwa ni kali, kipumuaji ikiwa una matatizo ya kupumua

  • Wakutunze hospitalini hadi upone

  • Kukupa dawa ili kuzuia maambukizi