Acetaminophen ni dawa ya dukani inayotumika kupunguza homa na maumivu. Inauzwa kwa majina mengi ya biashara, kama vile Tylenol. Hupatikana pia katika dawa nyingi za kutibu kukohoa na mafua.
Acetaminophen kwa kawaida ni salama, lakini matumizi kupita kiasi yanaweza kukudhuru.
Kuathiriwa na sumu ya acetaminophen ni nini?
Kuathiriwa na sumu yaAcetaminophen ni matokeo ya kutumia acetaminophen nyingi kupita kiasi.
Kuathiriwa na sumu ya Acetaminophen kunaweza kutokea unapokunywa dozi kupita kiasi kwa muda mfupi kama vile kutumia dawa au bidhaa mbalimbali zilizo na acetaminophen kwa bahati mbaya au ukitumia dozi kupita kiasi kimakusudi.
Athari ya sumu ya Acetaminophen inaweza pia kutokea polepole ikiwa unakunywa kipimo kikubwa kwa muda mrefu kwa sababu unakabiliwa na maumivu makali ya muda mrefu
Hata kipimo cha kawaida cha acetaminophen kinaweza kuwa hatari katika hali fulani kama vile ikiwa una uharibifu wa ini
Sumu ya Acetaminophen inaweza kuharibu ini lako na kusababisha ini kushindwa kufanya kazi
Sumu ya Acetaminophen inaweza kosa kuonyesha dalili hadi ini lako litakapoharibiwa
Soma lebo za dawa za kikohozi na mafua kwa makini
Soma lebo ya dawa za kupunguza maumivu na usikunywe zaidi ya dozi iliyopendekezwa
Ikiwa unamtunza mtoto mwenye mafua au kikohozi, kuwa mwangalifu sana ili usije ukampa mtoto acetaminophen kupita kiasi. Aina nyingi tofauti za dawa katika aina zote tofauti (kioevu, tembe, inayoweza kutafunwa) zina acetaminophen kama kiungo. Usimpe mtoto dawa yenye acetaminophen ikiwa mtoto tayari ametumia dawa tofauti yenye acetaminophen.
Ikiwa unafikiri wewe au mtu mwingine anaweza kuwa ameathiriwa na sumu ya acetaminophen, piga simu kwa usaidizi wa dharura (911 katika maeneo mengi nchini Marekani) mara moja au piga simu kwenye kituo cha kudhibiti sumu kwa ushauri (1-800 -222-1222 nchini Marekani). Shirika la Afya Duniani hutoa orodha ya kimataifa ya vituo vya sumu.
Je, dalili za mtu aliyeathirika na sumu ya acetaminophen ni zipi?
Kwa kawaida hakuna dalili mara moja.
Ikiwa utatumia dozi nyingi sana kupita kiasi, dalili hutokea kwa hatua:
Kwanza, unaweza kutapika na vinginevyo kuhisi mgonjwa
Baada ya siku 1 hadi 3, unaweza kuhisi mgonjwa tumboni mwako, kutapika, na kuwa na maumivu ya tumbo
Baada ya siku 3 hadi 4, unaweza kutapika zaidi, kuwa na ngozi na macho ya manjano (homa ya nyongo ya manjano), na kutokwa na damu chini ya ngozi, na kwenye pua au fizi
Baada ya siku kama 5, unaweza kupata nafuu au viungo vikose kutofanya kazi, hali ambayo inaweza kufanya uage dunia
Ikiwa sumu inatokana na kunywa vipimo vidogo kwa muda mrefu, dalili za kwanza zinaweza kuwa ini kutofanya kazi:
Ngozi na macho ya manjano (homa ya nyongo ya manjano)
Kuvuja Damu
Je madaktari wanawezaje kujua ikiwa nimeathirika na sumu ya acetaminophen?
Madaktari watafanya vipimo vya damu ili kuangalia kama kuna sumu ya acetaminophen. Wanaweza pia kufanya vipimo ili kuangalia ikiwa ini lako linafanya kazi vizuri.
Je, madaktari hutibu mgonjwa aliyeathirika na sumu ya acetaminophen vipi?
Madaktari watafanya:
Kukupa makaa hai ili kuzuia acetaminophen kuingia kwenye damu yako, ikiwa ulimeza acetaminophen ndani ya saa chache zilizopita.
Kukupa dawa ya kuzuia athari ya sumu (dawa inayofanya kazi dhidi ya acetaminophen) ili kulinda ini lako
Ikiwa ini lako limeharibiwa, unaweza kuhitaji kutibiwa tatizo la ini kushindwa kufanya kazi au hata kupokea upandikizaji wa ini.
Je, ninawezaje kuzuia athari ya sumu ya acetaminophen?
Kunywa dozi iliyopendekezwa tu
Soma lebo za dawa kwa uangalifu
Usinywe dawa iliyo na acetaminophen ikiwa tayari umetumia acetaminophen
Ikiwa una matatizo ya ini au unakunywa pombe, muulize daktari wako dawa unayopaswa kutumia kwa ajili ya maumivu au homa