Chuma ni madini ambayo mwili wako unahitaji; multivitamini zina chuma.
Je, athari ya sumu ya chuma ni nini?
Sumu ya chuma hutokana na matumizi ya kiasi kikubwa cha chuma jambo ambalo linadhuru mwili. Unapata athari ya sumu ya madini ya chuma kwa kumeza vidonge vingi vilivyo na madini ya chuma, kama vile multivitamini. Sumu ya chuma hutokea mara nyingi kwa watoto wadogo.
Sumu ya madini chuma ni mojawapo ya sababu kuu za vifo vya sumu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 5
Weka dawa zilizo na madini ya chuma na multivitamini mbali na watoto
Dalili za sumu kali kwa kawaida huonekana ndani ya masaa 6, lakini omba usaidizi mara moja, hata kama dalili bado hazijaonekana
Watu walio na sumu ya chuma wanahitaji kutunzwa hospitalini
Piga simu kwa usaidizi wa dharura wa matibabu (911 katika maeneo mengi ya Marekani) mara moja ikiwa unafikiri wewe au mtu mwingine anaweza kuwa na sumu ya chuma.
Je, dalili za athari ya sumu ya chuma ni zipi?
Dalili za kwanza kawaida hutokea ndani ya masaa 6:
Kutapika (inaweza kujumuisha kutapika damu)
Kuharisha (kutokwa kinyesi chepesi chenye umajimaji na kinachotoka mara kwa mara)
Kuudhika
Kupatwa na usingizi kila mara
Ikiwa sumu ni kali, dalili za mapema pia ni pamoja na:
Kupumua haraka
Mapigo ya moyo ya haraka
Kupoteza fahamu (kukosa fahamu na kutoweza kuamka)
Matukio ya kifafa (wakati mwili wako unasonga na kutetemeka ghafla bila udhibiti wako)
Wakati mwingine, unaweza kuonekana kama unapata nafuu kwa muda. Kisha, masaa 12 hadi 48 baada ya kunywa dozi kupita kiasi, una:
Homa
Mshtuko (kupungua sana kwa shinikizo la damu)
Kuvuja Damu
Macho na ngozi ya manajano (homa ya nyongo ya manjano)
Kuchanganyikiwa
Kupoteza fahamu
Kisha, ini lako hushindwa kufanya kazi na unaweza kufa kwa mshtuko, kutokwa na damu, na matatizo ya kuganda kwa damu.
Ikiwa utaokoka, takriban wiki 2 hadi 5 baada ya kunywa sumu kupita kiasi, dalili zako zinaweza kurudi. Huenda ukahisi:
Maumivu ya tumbo kukakamaa
Kuumwa tumboni mwako
Dalili hizi hutokea wakati tumbo lako na matumbo huzibwa kwa makovu.
Je, madaktari wanawezaje kujua kuwa nimeathiriwa na sumu ya chuma?
Madaktari wanaweza kupima kiwango cha chuma katika damu yako. Katika baadhi ya matukio, wanaweza kufanya eksirei kutafuta vidonge vilivyomezwa.
Je, madaktari hutibu aje sumu ya chuma?
Madaktari watakuuliza ukae hospitalini kwa matibabu.
Watakupa:
Mchanganyiko maalum wa kuosha vidonge vilivyobaki kwenye tumbo lako au matumbo
Dawa inayoshikamana na chuma, hivyo kuruhusu chuma kuondoka mwilini mwako kupitia mkojo (mkojo)