Athari ya Sumu Dawa ya Kuua Wadudu

Imepitiwa/Imerekebishwa Dec 2023

Dawa ya wadudu (dawa) ni dutu inayotumika kuua wadudu. Sumu (toksini) iliyo kwenye dawa za wadudu inaweza kukufanya mgonjwa.

Je, sumu ya dawa ya wadudu ni nini?

Sumu ya dawa ya wadudu ni maradhi yanayotokana na kumeza, kuvuta ndani, au kugusa sana dawa ya wadudu.

  • Ikiwa dawa ya wadudu itaingia kwenye nguo au ngozi yako, vua nguo zako na uoshe ngozi yako mara moja

  • Unaweza kukohoa na kuwa na matatizo ya kupumua

  • Daktari wako atachukua sampuli ya damu yako ili kuangalia kama ina dawa ya wadudu

  • Kuna dawa nyingi za kutibu sumu ya dawa ya wadudu

Piga simu kwa msaada wa dharura wa matibabu (911 katika maeneo mengi ya Marekani) ikiwa wewe au mtu mwingine anaweza kuwa na sumu ya dawa ya wadudu, au piga simu kituo cha kudhibiti sumu kwa ushauri (1-800-222-1222 nchini Marekani). Shirika la Afya Duniani hutoa orodha ya kimataifa ya vituo vya sumu.

Je, dalili za athari za sumu ya dawa ya wadudu ni zipi?

Dalili hutegemea aina ya dawa ya wadudu iliyokupa sumu. Kuna aina mbili kuu za dawa za wadudu:

  • Organofosfeti na kabameti

  • Pirethrini

Organofosfeti na kabameti zinaweza kusababisha:

  • Macho yaliyojaa machozi au uoni hafifu

  • Kutokwa jasho

  • Mate zaidi (tema) kinywani mwako

  • Kukohoa

  • Kutapika

  • Kutoa haja kubwa mara kwa mara (kinyesi) au kukojoa (mkojo)

  • Kiwango cha mapigo ya moyo kisicho cha kawaida

  • Kupumua kwa shida

Pirethrini huwa na kiasi kidogo cha sumu kwa watu. Dalili za sumu ya pirethrini ni pamoja na:

  • Kupiga chafya

  • Macho yenye majimaji

  • Kukohoa

  • Matatizo ya kupumua, wakati mwingine

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nimeathiriwa na sumu na dawa ya kuua wadudu?

Madaktari watashuku sumu ya dawa ya kuua wadudu kulingana na dalili zako na maelezo yako ya kile kilichotokea. Wakati mwingine wanaweza kupima damu yako ili kujua ikiwa una sumu ya dawa ya kuua wadudu.

Je, madaktari hutibu aje mgonjwa aliyeathiriwa na sumu ya dawa ya kuua wadudu?

Madaktari watakuamuru uvue nguo yoyote iliyogusa dawa na uoshe ngozi yako. Watakupa dawa kulingana na dalili zako kwa kuzingatia aina ya dawa ya kuua wadudu iliyokupa sumu.