Je, sumu ya vyakula vya baharini ni nini?
Vyakula fulani vya baharini huwa na kemikali zenye sumu. Sumu ya vyakula vya baharini hutokea pale ambapo unaugua kwa kula samaki fulani au samakigamba ambao wana toksini (sumu).
Je, dalili za sumu ya vyakula vya baharini ni zipi?
Dalili hutegemea aina ya sumu iliyo kwenye samaki.
Sumu ya Ciguatera
Ciguatera ni aina ya toksini ambayo inaweza kujilimbikiza katika samaki wenye umri mkubwa. Kupika samaki hakuondoi toksini.
Masaa 2 hadi 8 baada ya kula samaki, unahisi:
Kuumwa tumboni mwako
Kukakamaa kwa tumbo
Kuharisha (kutokwa kinyesi chepesi cha majimaji na kinachotoka mara kwa mara)
Baadaye, unahisi:
Mwasho
Kudungwadungwa miguu na mikono
Maumivu ya kichwa
Maumivu ya misuli
Kuhisi mwili una joto na baridi sana kwa wakati mmoja
Maumivu kwenye uso
Dalili zinaweza kudumu kwa miezi kadhaa.
Sumu ya totovu
Totovu (fugu) huwa na sumu hatari Kupika au kugandisha samaki hakuondoi toksini.
Unahisi:
Kuumwa tumboni mwako
Kukakamaa kwa tumbo
Kuhara (kinyesi cha mara kwa mara, cha majimaji, au kilicholegea)
Kupooza (kushindwa kusogeza misuli yako)—hii inaweza kukufanya ushindwe kupumua na kufariki
Ikiwa unafikiria kuwa wewe au mtu mwingine anaweza kuwa na sumu ya totovu, piga simu kwa usaidizi wa dharura wa matibabu (911 kwenye maeneo mengi nchini Marekani) au nenda hospitalini mara moja.
sumu ya skambroidi
Sumu inayotoka kwenye samaki mwenye histamini nyingi ni sumu ambayo hukua katika aina fulani za samaki (makareli, tuna, na bonito) ikiwa samaki hawatahifadhiwa au kuhifadhiwa kwenye jokofu ipasavyo.
Samaki wanaweza kuwa na ladha ya chungu au pilipili.
Dalili za sumu ya skambroidi:
Ngozi yenye wekundu na yenye joto (kuiva kwa ngozi)
Kuhisi mgonjwa tumboni
Kutapika
Mizinga (vipele vya ngozi vyekundu vinavyotokea ghafla)
Sumu ya samakigamba
Sumu ya samakigamba hutokana na kula samakigamba, kama vile kamba wa baharini, kongwe, chaza na kapu, ambao wana sumu inayoitwa saxitoxin.
Kupika samakigamba hakuzuii sumu.
Dalili za sumu ya samakigamba:
Hisia za kuchomwa na kudungwadungwa karibu na mdomo baada ya dakika chache za kula
Kuhisi mgonjwa tumboni
Kutapika
Kukakamaa kwa tumbo
Udhaifu wa misuli
Kutoweza kusongeza misuli ya mkono na mguu
Kupumua kwa shida
Je, madaktari hutibu vipi sumu ya vyakula vya baharini vilivyoganda?
Matibabu maalum hulingana na aina ya sumu.
Madaktari watafanya:
Watakupa dawa (antihistamini)
kukufanya kula vyakula majimaji kwa wingi
Watakuongezea maji ya IV (kwenye mshipa wako wa damu), ikiwa huwezi kunywa
Kukupa dawa ili kukomesha kutapika, ikiwa inahitajika
Kukupa dawa ya kurudisha joto la mwili na mapigo ya moyo na upumuaji katika hali ya kawaida