Aspirini ni dawa inayouzwa dukani ambayo hutumiwa kutuliza maumivu.
Je, sumu ya aspirini ni nini?
Sumu ya Aspirini ni maradhi yanayotokana na kutumia dozi zaidi ya aspirini kwa wakati mmoja, au dozi nyingi za chini za aspirini kwa kipindi kirefu cha muda (kupatwa na sumu polepole).
Ili kuwa na sumu ya aspirini, unahitaji kutumia zaidi ya kiwango cha kawaida
Kutumia kiwango kidogo cha aspirini (aspirini ya watoto) kila siku kulingana na maagizo ya daktari wako ili kupunguza uwezekano wa shambulio la moyo hakuwezi kusababisha kupatwa na sumu polepole
Watoto hawapaswi kamwe kupewa aspirini kwa sababu inaweza kusababisha ugonjwa nadra lakini unaohatarisha maisha unaoitwa Ugonjwa wa Reye
Mafuta ya wintergreen yana kemikali inayohusiana na aspirini ndani yake Ni hatari sana kwa watoto wadogo na yanaweza kuwaua wakimeza hata kijiko kimoja.
Ikiwa unafikiri wewe au mtu mwingine anaweza kuwa ameathiriwa na sumu ya aspirini, piga simu kwa usaidizi wa dharura (911 katika maeneo mengi nchini Marekani) mara moja au piga simu kwenye kituo cha kudhibiti sumu kwa ushauri (1-800 -222-1222 nchini Marekani). Shirika la Afya Duniani hutoa orodha ya kimataifa ya vituo vya sumu.
Je, dalili za athari ya sumu ya aspirini ni zipi?
Ukitumia aspirini nyingi kupita kiasi kwa wakati mmoja (sumu kali), dalili za kwanza ni:
Kuhisi mgonjwa tumboni
Kutapika
Kupumua haraka sana
Mlio katika masikio yako
Kutokwa jasho
Kwa sumu kali, unaweza pia kuhisi:
Kuhisi kizunguzungu
Dalili za homa
Kuwa na usingizi usio wa kawaida au mwenye nguvu zaidi (mchangamfu)
Mwili wako unasogea na kutetemeka ghafla bila udhibiti wako (matukio ya kifafa)
Kana kwama una matatizo ya kupumua
Dalili za kupatwa na sumu polepole huonekana baada ya siku au wiki kadhaa. Unahisi:
Kuhisi usingizi
Kuchanganyikiwa
Kuhisi kuwa unaona au kusikia vitu ambavyo havipo (ndoto)
Kizunguzungu au kichwa kuwa chepesi
Kuhisi kana kwamba una matatizo ya kupumua au kupumua kwako ni kwa haraka sana
Je, madaktari wanawezaje kujua kama nimeathiriwa na sumu ya aspirini?
Madaktari watachukua sampuli ya damu ili kupima kiasi cha aspirini katika damu yako.
Je, madaktari humtibu aje mgonjwa aliye na athari ya sumu ya aspirini?
Madaktari watafanya:
Kukupa makaa hai ili kuzuia aspirini kuingia kwenye damu yako
Kukudungia maji ndani ya mishipa ya damu (kwenye mshipa wako), ikihitajika
Kwa athari kali ya sumu, kutumia mashine maalum kuchuja aspirini kutoka kwa damu yako
Kutibu dalili zako zingine kadri zinavyotokea