Kuvunjika kwa Mifupa ya Chini ya Miguu

(Mguu Uliovunjika; Mvunjiko wa Mifupa ya Vidole vya Mguu)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2025

Mivunjiko ya mifupa ya vidole vya mguu ni nini?

Mifupa ya vidole vya miguu ni mifupa 5 mirefu katikati ya mguu wako. Mifupa hii huunganisha sehemu ya nyuma ya mguu wako kwenye vidole. Mivunjiko yake ni pale ambapo mifupa hii huvunjika. Mifupa yote iliyovunjika inachukuliwa kuwa iliyoharibika. Kwa maelezo zaidi, angalia Muhtasari kuhusu Mifupa Iliyovunjika.

Nini husababisha kuvunjika kwa mifupa ya mguu?

Kuvunjika kwa mifupa ya mguu kunaweza kusababishwa na:

  • Kupinda kwa mguu wako

  • Nguvu kubwa (kama vile kitu kizito kugonga mguu wako)

  • Mikazo midogomidogo ya mara kwa mara, (kama vile kutembea masafa marefu)—hii inaitwa mvunjiko wa mkazo

Mivunjiko ya mkazo ni nini kwenye mifupa ya mguu?

Mivunjiko ya mkazo ni mivunjiko midogo inayotokana na kutumia mfupa zaidi. Hutokea sana kwenye mifupa ya miguu.

  • Mivunjiko ya mkazo ni mivunjiko mifdogo kwenye mfupa, sio mivunjiko kamili

  • Husababishwa na kutembea au kukimbia sana

  • Utapata maumivu na hisia za uchungu, hasa unaposimama

  • Madaktari wanaweza kujua kama una mivunjiko ya mkazo kwa kuchunguza eksirei (ingawa wakati mwingine huchukua wiki chache ili ionekane kwenye eksirei) au uchanganuzi wa CT au MRI

  • Utatumia magongo na kupumzisha mguu wako wakati unaendelea kupona

Mvunjiko wa Mkazo ni nini?

Mivunjiko ya mkazo ni mivunjiko midogomidogo kwenye mfupa inayosababishwa na mgongano wa mara kwa mara.

Mteguko wa Lisfranc ni nini?

Mvunjiko wa Lisfranc ni aina maalum ya mvunjiko wa mifupa ya chini ya mguu.

  • Hutokea kwa mfupa wa 2 wa mnogowiko (mfupa unaounganisha sehemu ya nyuma ya mguu wako na kidole chako cha 2 cha mguu)

  • Husababishwa na kuanguka au kuteguka kwa mguu, au mguu wako kugongwa kwa nguvu

  • Wachezaji wa kandanda, waendesha pikipiki, na wapanda farasi wana uwezekano mkubwa wa kupata mteguko wa Lisfranc.

  • Wakati mwingine utahisi maumivu mguuni na michubuko chini ya mguu

  • Madaktari hufanya uchanganuzi wa eksirei au CT

  • Madaktari hufanya upasuaji ili kurejesha mifupa mahali pake

Mteguko wa Lisfranc ni mbaya na unaweza kusababisha maumivu na ugonjwa wa baridi yabisi. Huenda ukalazimika kuacha kucheza michezo fulani hata baada ya kupona.

Mteguko wa Lisfranc

Mfupa wa 2 wa mnogowiko kuvunjika sehemu ya chini na vipande vilivyovunjika kutenganishwa (kuteguka). Jeraha hili linaitwa Mteguko wa Lisfranc

Mivunjiko ya mfupa wa 5 wa mnogowiko ni nini?

Mfupa wa 5 wa mnogowikoni ni mfupa mrefu unaounganisha sehemu ya nyuma ya mguu wako na kidole chako kidogo cha mguu. Mvunjiko wa mfupa wa 5 wa mnogowiko ni kuvunjika kwa mfupa huu.

  • Ni moja ya mivunjiko ya kanyagio inayotokea zaidi

  • Mvunjiko unaweza kuwa karibu na kifundo cha mguu (chini) au katikati ya mfupa (katikati)

  • Inaweza kutokea kwa sababu ya mkazo (kutumika kupita kiasi) au jeraha moja

  • Unaweza kuwa na maumivu pembeni mwa mguu wako

  • Madaktari hugundua ikiwa umevunjika kwa kutumia eksirei

  • Utajitaji magongo na kiatu kigumu cha kukulinda au buti maalumu

  • Mara chache, utahitaji kasti au upasuaji