Hali ya Shinikizo na Uvimbe Mwilini ni nini?
Hali ya shinikizo na uvimbe mwilini ni kuongezeka kwa shinikizo kutokana na misuli iliyovimba, iliyojeruhiwa ambayo huzuia mtiririko wa damu kwenye misuli hiyo na misuli iliyo karibu nazo.
Katika baadhi ya sehemu za mwili wako, safu ngumu ya tishu hufunika kundi la misuli, neva, na mishipa ya damu. Tishu zilizofunikwa kinaitwa tishu inayofunikwa. Msuli uliojeruhiwa ndani ya tishu unayofunikwa ikivimba, tishu ngumu inaweza isinyooke vya kutosha kuruhusu uvimbe unaohitajika na misuli. Badala yake, uvimbe huongeza shinikizo kwenye tishu iliyofunikwa na inaweza kukata mtiririko wa damu. Bila damu, tishu iliyofunikwa hufa.
Hali ya Shinikizo na Uvimbe Mwilini ni nadra, lakini ni matatizo hatari sana ya majeraha fulani
Mara nyingi hutokea kutokana na mfupa uliovunjika kwenye mkono wa chini au mguu wa chini
Dalili kuu ni maumivu makali, yanayozidi katika sehemu ya mwili iliyojeruhiwa
Usipopata matibabu, misuli hufa na utapata gangrini
Madaktari hufanya upasuaji ili kukata safu ngumu ya tishu na kufunua tishu zilizofunikwa, jambo hili hupunguza shinikizo
Usipopata matibabu mapema vya kutosha, madaktari wanaweza kuhitaji kukata (kuondoa) kiungo chako
Hali ya Shinikizo na Uvimbe Mwilini husababishwa na nini?
Hali ya shinikizo na uvimbe mwilini kwa viungo husababishwa na:
Kuvunkika kwa mfupa(Mvunjiko) hasa wa mguu wa chini
Jeraha ambalo linahusishwa kupondwa kwa mkono au mguu wako
Mara chache, hali ya shinikizo na uvimbe mwilini husababishwa na:
Bendeji au plasta inayokubana
Kuumwa na nyoka
Kuchomeka
Kupitiliza dozi ya dawa
Dalili za hali ya shinikizo na uvimbe mwilini ni zipi?
Dalili kuu ni:
Maumivu makali sana kwenye sehemu ya mwili iliyojeruhiwa ambayo huzidi kuongezeka—maumivu huwa makali zaidi kuliko vile unavyotarajia kutokana na jeraha.
Huenda pia:
Maumivu unaposogeza vidole vya mkono au mguu uliojeruhiwa
Maumivu makali sana hivi kwamba dawa hazisaidii
Kufa ganzi kwenye vidole vya mkono au mguu uliojeruhiwa
Ngozi iliyokwajuka, kukazika na kuwa baridi
Madaktari wanawezaje kujua kama nina hali ya shinikizo na uvimbe mwilini?
Madaktari watafanya:
Kwa kuangalia vipigo vya mishipa ya damu kwenye sehemu ya mwili ambapo umejeruhiwa
Kwa kuweka sindano kwenye kiungo chako kilichojeruhiwa ili kupima shinikizo katika eneo karibu na misuli
Madaktari hutibu vipi hali ya shinikizo na uvimbe mwilini?
Madaktari watafanya:
Kwa kutoa bendeji, plasta, au kitu chochote kinachoweka shinikizo kwenye sehemu ya mwili
Kwa kawaida watafanya upasuaji ili kukata eneo lenye shinikizo, na huku kutapunguza shinikizo na kuruhusu damu kufikia misuli yako
Ikiwa tishu zako zimekufa, huenda sehemu hiyo ya mwili ikahitaji kukatwa (kuondolewa)
Ni muhimu sana kupata matibabu ya ugonjwa wa hali ya shinikizo na uvimbe mwilini mara moja, kwa sababu inaweza kusababisha maambukizi yanayoweza kuhatarisha maisha katika mkono au mguu wako.