Kuvunjika kwa Fupanyonga

(Mvunjiko wa Fupanyonga)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Mvunjiko wa fupanyonga ni nini?

Fupanyonga ni pete kubwa, lenye mifupa inayounganisha miguu yako na mgongo wako. Ina mifupa kadhaa tofauti inayoshikiliwa pamoja na kano. Mfupa wowote kwenye fupanyonga unaweza kuvunjika. Mifupa yote iliyovunjika inachukuliwa kuwa iliyoharibika. Kwa maelezo zaidi, angalia Muhtasari kuhusu Mifupa Iliyovunjika.

  • Kuvunjika kwa fupanyonga kunaweza kuwa hatari sana kulingana na mifupa iliyovunjika na jinsi ilivyovunjika

  • Fupanyonga iliyovunjika ni chungu, hata wakati umeketi au umelala

  • Fupanyonga linapovunjika vibaya linaweza kusababisha kutokwa na damu nyingi na majeraha mengine ya ndani

  • Kulingana na aina ya mvunjiko, madaktari wanaweza kutibu kwa mapumziko ya kitandani pekee au unaweza kuhitaji upasuaji

Mivunjiko ya Fupanyonga

Mivunjiko (iliyoonyeshwa kwa rangi nyekundu hapa chini) inaweza kutokea kwenye mifupa ya ilium, pubis, au ischium.

Ni nini husababisha kuvunjika kwa fupanyonga?

Kwa vijana, kuvunjika kwa fupanyonga kwa kawaida husababishwa na:

  • Ajali za kuendesha gari au pikipiki kwa kasi

  • Kugongwa na gari

  • Kuanguka kutoka mahali pa juu

  • Majeraha ya michezo

Watu wazee wanaweza kuvunjika fupanyonga kutokana na jeraha lisilo kali sana, kama vile kuanguka:

  • Wanapotoka nje ya bafu

  • Wanaposhuka chini ya ngazi

  • Wanapoangushwa na kitu fulani wanapotembea

Ugonjwa wa kudhoofu kwa mifupa hudhoofisha mifupa yako na kufanya fupanyonga lako livunjike iwapo utaanguka.

Dalili za kuvunjika kwa fupanyonga ni zipi?

Mara nyingi kuvunjika kwa fupanyonga husababisha:

  • Maumivu katika eneo la kinena, hata wakati umeketi au umelala

  • Maumivu makali unapojaribu kutembea

  • Kuvimba na michubuko

  • Wakati mwingine, damu kwenye mkojo, ugumu wa kukojoa, au kutokwa na damu kutoka kwenye eneo la kinena

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa fupanyonga yangu imevunjika?

Madaktari hufanya:

Madaktari hutibu vipi mvunjiko wa fupanyonga?

Madaktari watatibu mivunjiko midogo ya fupanyonga kwa kukuagiza:

  • Kupumzika kitandani kwa muda mfupi

  • Meza dawa ya maumivu

  • Kusimama na kutembea haraka uwezavyo

Madaktari hutibu mivunjiko mikubwa ya fupanyonga kwa kuimarisha fupanyonga kwanza kwa kuifunga kwa kitambaa au kamba. Kisha madaktari watafanya haya:

  • Wakati mwingine watafanya upasuaji ili kurejesha mifupa mahali pake na kutumia skurubu na vipande vya chuma ili kuishikilia

  • Wakati mwingine watatumia kirekebishaji cha nje, chuma ambayo imeunganishwa na mwili wako kwa skurubu ndefu kupitia kwenye ngozi yako hadi kwenye mifupa.

Ikiwa bado unatokwa na damu nyingi, daktari wako anaweza kujaribu:

  • Embolisesheni: Daktari wako atadunga mishipa ya damu inayovuja dutu ambayo inaweza kuziba mshipa na kuzuia uvujaji wa damu

  • Upakiaji wa fupanyonga: Daktari wako atakufanyia upasuaji wa kuweka vitu fulani kwenye eneo la fupanyonga ambavyo vinafyonza damu na kuweka shinikizo kwenye mishipa ya damu ili kusaidia kusitisha uvujaji wa damu—mara tu uvujaji wa damu unapokoma siku chache baadaye, daktari atakufanyia upasuaji tena ili kutoa vitu hivyo na kurekebisha mifupa yako ya fupanyonga iliyovunjika

Baada ya mfupa uliovunjika kupona, utahitaji kufanya mazoezi ili kurejesha nguvu zako.