Kuvunjika kwa Bega

(Muungabega Uliovunjika)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Kuvunjika kwa bega ni nini?

Mvunjiko wa bega ni kuvunjika karibu na sehemu ya juu ya mkono wako wa juu, karibu na kiungo cha bega lako. Mfupa huu unaitwa muungabega. Mifupa yote iliyovunjika inachukuliwa kuwa iliyoharibika. Kwa maelezo zaidi, angalia Muhtasari kuhusu Mifupa Iliyovunjika.

Mvunjiko wa bega

Mivunjiko hutokea kwenye sehemu ya juu ya mfupa wa mkono wa juu (muungabega) husababisha maumivu kwenye bega kwa sababu mfupa wa juu wa mkono ni sehemu ya kiungo cha bega. Mfupa wa sehemu ya juu ya mkono unaweza kuvunjika katika sehemu tofauti. Mfano mmoja umeonyeshwa hapa chini.

  • Visa vingi vya kuvunjika kwa bega ni pale unapoanguka na mkono wako ukiwa umenyooshwa

  • Kuvunjika kwa mabega hutokea sanasana kwa watu wazee

  • Utapata maumivu na huenda usiweze kusogeza mkono wako begani

  • Mara nyingi, utahitaji tu kufungwa tanzi kwenye mkono, lakini wakati mwingine madaktari hufanya upasuaji

Ni nini husababisha kuvunjika kwa bega?

Sababu za kawaida:

  • Kugongwa kwa nguvu kwa sehemu ya juu ya mkono

  • Kuanguka mkono wako ukiwa umenyooshwa

Dalili za mvunjiko wa bega ni zipi?

Dalili zinajumuisha:

  • Maumivu na uvimbe kwenye bega

  • Ugumu wa kuinua mkono wako

  • Wakati mwingine, mkono wako wa juu kufa ganzi

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa bega langu limevunjika?

Madaktari hufanya:

Madaktari hutibu vipi mvunjiko wa bega?

Madaktari hutibu mvunjiko wa bega kwa:

  • Tanzi, na wakati mwingine pia bendeji (kamba ambayo inashikilia tanzi kwenye mwili wako)

  • Mazoezi ya kuzuia bega lako kukazika

  • Wakati mwingine, upasuaji kwa mivunjiko mibaya

Ikiwa unahitaji upasuaji, daktari wa upasuaji anaweza kutumia vipande, skurubu, au waya ili kushikilia mifupa yako huku ikiendelea kupona. Wakati mwingine, daktari wa upasuaji ataweka kiungo bandia cha bega (ubadili wa kiungo).

Baada ya mfupa uliovunjika kupona, bega lako litakuwa gumu. Utahitaji kufanya mazoezi ili kuilegeza na kupata nguvu zako tena.