Mivunjiko kwenye Maeneo ya Ukuaji

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Mivunjiko ya kwenye maeneo ya ukuaji ni nini?

Mvunjiko ni kuvunjika kwa mfupa.

Maeneo ya Ukuaji ni maeneo ya gegedu karibu na mwisho wa mfupa. Maeneo ya Ukuaji ni mahali ambapo mifupa hukua. Ni watoto na vijana pekee ndio wana maeneo ya ukuaji kwenye mifupa, kwa sababu baada ya mifupa kukua, maeneo hayo hugeuka kuwa mfupa wa kawaida.

Kutafuta Maeneo ya Ukuaji

Maeneo ya ukuaji (yanayoonyeshwa na mistari ya rangi ya waridi) ni maeneo ya gegedu karibu na ncha za mifupa mirefu, kama vile mifupa ya mkono na mguu. Huwezesha mifupa kurefuka hadi watoto wafikie urefu wao kamili.

  • Mvunjiko wa eneo la ukuaji ni kuvujika upande hadi upade au juu hadi chini kwenye eneo la ukuaji

Gegedu ni laini kuliko mfupa kwa hivyo huvunjika kwa urahisi zaidi.

  • Ni watoto na vijana pekee ndio hupata mivunjiko ya maeneo ya ukuaji—kwa watu wazima mfupa huingia pale ambapo maeneo ya ukuaji yalikuwepo.

  • Kuvunjika kwenye eneo la ukuaji huumiza na kuvimba kama kuvunjika kwa mfupa wa kawaida

  • Kuvunjika kwenye eneo la ukuaji kunaweza kuzuia mfupa isikue au kuufanya ukue ukiwa umepinda

  • Mtoto wako atahitaji plasta au banzi

  • Mara chache, madaktari watafanya upasuaji ili kurejesha mifupa mahali pake

Ni nini husababisha mivunjiko ya maeneo ya ukuaji?

Mivunjiko ya maeneo ya ukuaji hutokana na:

  • Mgongano wenye nguvu, kama vile kuanguka au ajali ya gari

  • Mkazo kwenye mifupa kutokana na harakati za kurudiarudia

Watoto wanaofanya mazoezi ya viungo, kucheza besiboli, au kukimbia masafa marefu wana uwezekano mkubwa wa kupata mivunjiko ya maeneo ya ukuaji.

Dalili za mivunjiko ya maeneo ya ukuaji ni zipi?

Dalili zinajumuisha:

  • Maumivu, hasa eneo hilo linapoguswa

  • Kuvimba

  • Tatizo la kusogeza sehemu ya mwili iliyojeruhiwa au unapoweka uzito juu yake

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa mtoto wangu ana mvunjiko wa maeneo ya ukuaji?

Ili kujua ikiwa mtoto wako amevunjika eneo la ukuaji, madaktari hufanya haya:

Madaktari hutibu vipi mivunjiko ya maeneo ya ukuaji?

Madaktari hutibu mivunjiko ya maeneo ya ukuaji kwa:

  • Kusogeza mifupa kwa upole irudi kwenye mahali pake

  • Kutumia banzi au plasta ili kurejesha mifupa kwenye mahali pake inapopona

  • Wakati mwingine, kufanya upasuaji na kushikilia mifupa kwa kutumia pini, skurubu, fito, au vipande vya chuma.

Kugandamizwa kwa maeneo ya ukuaji husababisha matatizo ya ukuaji wa mfupa. Watoto waliovunjika kwenye eneo la ukuaji wanapaswa kwenda kwa daktari wa watoto (daktari ambaye ni mtaalamu wa kutibu mifupa, misuli na viungo vya watoto).