Kifundo cha mguu kimevunjika

(Mvunjiko wa kifundo cha mguu)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Mvunjiko wa kifundo cha mguu ni nini?

Kiungo cha kifundo cha mguu wako ni pale ambapo mifupa 2 mirefu kwenye mguu wako wa chini hukutana na mifupa midogo iliyo juu ya mguu wako. Mivunjiko ya mifupa yoyote hati hii inaweza kuchukuliwa kuwa kifundo cha mguu kilichovunjika. Lakini madaktari kwa kawaida husema "kifundo cha mguu kilichovunjika" mfupa mrefu ulio karibu na mguu unapovunjika. Mifupa yote iliyovunjika inachukuliwa kuwa iliyoharibika. Kwa maelezo zaidi, angalia Muhtasari kuhusu Mifupa Iliyovunjika.

  • Mivunjiko ya kifundo cha mguu hutokea mara nyingi

  • Kifundo chako kitavimba na kuwa na uchungu

  • Utahitaji kufungwa kwa banzi, plasta, au wakati mwingine upasuaji kulingana na hali ya mvunjiko ilivyo

Dalili za mvunjiko wa kifundo cha mguu ni zipi?

Dalili zinajumuisha:

  • Maumivu na uvimbe kwenye kifundo cha mguu wako

  • Kutoweza kuweka uzito kwenye mguu wako

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa kifundo cha mguu kimevunjika?

Madaktari hufanya:

Madaktari hutibu vipi mvunjiko wa kifundo cha mguu?

Madaktari watafanya:

  • Kurejesha mifupa zinapofaa ikiwa haijapangwa vizuri

  • Kukuvika banzi au plasta kwa muda wa wiki 6, hadi mifupa yako ipone

  • Ikiwa inahitajika, watafanya upasuaji ili kurejesha mifupa inapofaa na kuishikilia hapo kwa pini, fito, skurubu au vipande vya chuma.

Huenda ujahitaji matibabu ya mwili baada ya banzi au plasta kutolewa.

Ikiwa mifupa ikibaki kwenye mahali pake, kwa kawaida kifundo cha mguu hupona vizuri. Ikiwa mifupa itatoka kwenye nafasi yake, unaweza kupata ugonjwa wa baridi yabisi na kuwa na uwezekano mkubwa wa kupata mvunjiko mwingine wa kifundo cha mguu.