Kuvunjika kwa Kifundo cha Mkono

(Mvunjiko wa kifundo cha mkono)

Imepitiwa/Imerekebishwa Jan 2023

Mifupa yote iliyovunjika inachukuliwa kuwa iliyoharibika. Kwa maelezo zaidi, angalia Muhtasari kuhusu Mifupa Iliyovunjika.

Kuvunjika kwa kifundo cha mkono ni nini?

Kiungo cha kifundo cha mkono wako ni pale ambapo mifupa 2 mirefu kwenye kigasha hukutana na mifupa 8 midogo iliyo karibu na kiganja chako. Mivunjiko ya mifupa yoyote hati hii inaweza kuchukuliwa kuwa kifundo cha mkono kilichovunjika. Lakini madaktari kwa kawaida husema "kuvunjika kwa kifundo cha mkono" unapokuwa na:

  • Kuvunjika kwa mfupa mmoja au yote miwili kati ya 2 ya mkono wako

Aina hii ya kuvunjika kwa kifundo cha mkono ni jeraha linalotokea sana. Mivunjiko ya mifupa midogo ya kifundo cha mkono haitokei sana.

  • Kuvunjika kwa kifundo cha mkono huonekana sana kwa watu wazee

  • Mifupa inaweza kusukumwa ikatoka kwenye mahali pake na kuhitaji kurejeshwa

  • Kwa kawaida utahitaji plasta tu, lakini wakati mwingine madaktari hufanya upasuaji

Nenda kwa daktari mara moja ikiwa unafikiri kuwa kifundo cha mkono wako kimevunjika.

Ni nini husababisha kuvunjika kwa kifundo cha mkono?

Mivunjiko ya kifundo cha mkono mara nyingi husababishwa na:

  • Kujikinga usianguke kwa kutua kwenye kiganja chako au nyuma ya mkono wako

Mivunjiko ya Kifundo cha Mkono

Dalili za mvunjiko wa kifundo cha mkono ni zipi?

Unaweza kupata dalili zifuatazo:

  • Mkono wako unavimba na una maumivu

  • Kuhisi uchungu unapozungusha kifundo cha mkono wako

  • Kifundo cha mkono wako kinaweza kuonekana kuwa na muundo usio wa kawaida

  • Wakati mwingine, ncha ya kidole chako cha shahada inaweza kufa ganzi au matatizo ya kugusa kidole gumba kwa kidole cha mwisho

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa kifundo cha mkono wako kimevunjika?

Madaktari hufanya:

Madaktari hutibu vipi mvunjiko wa kifundo cha mkono?

Madaktari watafanya:

  • Kukupa dawa ya maumivu

  • Kurejesha mifupa yako mahali pake

  • Kukuvika plasta kwa muda wa wiki kadhaa

  • Wakati mwingine, watafanya upasuaji ili kurejesha mifupa na kuziweka kwenye mahali pake

  • Wakati mwingine, watatumia kipande cha chuma au kirekebishaji cha nje (chuma inayowekwa nje ya mwili wako kwa skrubu ndefu zinazounganishwa na mifupa yako) ili mifupa yako ikae mahali ambapo itapona vizuri.

Baada ya mfupa uliovunjika kupona, kifundo cha mkono wako kitakuwa kigumu. Utahitaji kufanya mazoezi ili kuilegeza na kupata nguvu zako tena.