Perema za Mkole wa Kifua

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2023

Perema ya mkole wa kifua ni nini?

Kidari kinahusiana na kifua (kidari). Aota ndio mshipa mkuu wa damu (ateri) ambao hubeba damu kutoka kwenye moyo wako hadi sehemu nyingine zote za mwili. Perema ni uvimbe kwenye ukuta wa ateri. Perema ya mkole wa kifua ni uvimbe katika sehemu ya mkole wako ambayo hupitia kwenye kifua chako.

  • Perema ya mkole wa kifua inaweza kusababisha maumivu, kukohoa, na kuforota

  • Perema ikipasuka, damu humwagika na unapata maumivu makali na shinikizo la chini la damu

  • Perema ikipasuka husababisha kifo isipofanyiwa upasuaji

  • Madaktari hugundua perema kwa bahati mbaya wanapofanya uchunguzi wa picha (kama vile eskrirei au uchanganuzi wa CT) iliyochukuliwa kwa ajili ya tatizo lingine.

  • Madaktari hujaribu kurekebisha perema kwa upasuaji kabla ya perema kupasuka

Perema ya mkole wa kifua husababishwa na nini?

Vyanzo vya perema ya mkole wa kifua vinaweza kujumuisha:

Dalili za perema za mkole wa kifua ni zipi?

Inawezekana usipate dalili, hata kama perema zako ni kubwa sana.

Wakati mwingine, perema hubana ogani, mishipa, au misuli iliyo karibu nazo na kusababisha dalili, kama vile:

  • Maumivu katika sehemu ya juu ya mgongo wako

  • Kukohoa

  • Kukohoa damu

  • Matatizo ya kumeza

  • Sauti yenye kukwaruza

  • Mapigo yasiyo ya kawaida kwenye kifua chako

Dalili za perema yako kupasuka ni pamoja na:

  • Maumivu makali katika sehemu ya juu ya mgongo wako

  • Maumivu katika eneo la tumbo, kifua na mikono

  • Kushuka ghafla kwa shinikizo la damu (mshtuko)

  • Kuvuja damu kwa ndani

Perema ikipasuka husababisha kifo usipofanyiwa upasuaji.

Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina perema ya mkole wa kifua?

Madaktari watakuuliza kuhusu dalili zako au wanaweza kuona dalili za perema wakati wa uchunguzi wa kimwili, kama vile:

  • Kuvuma kwa moyo (sauti ya kishindo ambayo damu yako hutoa inapotoka nje ya moyo kwenda kwenye perema)

Eksirei iliyochukuliwa kwa sababu nyingine inaweza kuonyesha perema.

Madaktari watafanya vipimo vya picha ili kuona ukubwa wa perema na mahali ilipo haswa, kama vile:

Madaktari hutibu vipi perema ya mkole wa kifua?

Madaktari wataangalia ukubwa wa perema yako kila baada ya miezi 6 hadi 12 kwa kutumia uchanganuzi wa CT.

Ikiwa perema yako ni ndogo, madaktari wanaweza kukuagiza:

  • Kuepuka kuvuta sigara

  • Kumeza dawa za kudhibiti shinikizo la damu

Ikiwa una perema kubwa, utahitaji kufanyiwa upasuaji.

Upasuaji

Huenda daktari akafanya upasuaji wa kuingiza mrija (kupandikiza) kwenye aota yako ili kurekebisha sehemu yenye perema. Aina mbili za upasuaji zinawezekana. Daktari anaweza kukata kifua chako na kuweka kipandikizi. Au anaweza kuweka kipandikizi kwenye mkole wako kwa kupitia ateri iliyopo katika sehemu ya juu ya mguu wako. Aina ya upasuaji unaofanyiwa unategemea umri, hali ya afya, na sehemu ilipo perema ya mkole wako.

Perema ikipasuka au ikikaribia kupasuka, upasuaji wa dharura unaweza kuokoa maisha yako. Utafariki dunia usipofanyiwa upasuaji.