Mgawanyiko wa Mkole

Imepitiwa/Imerekebishwa Feb 2023

Mgawanyiko wa mkole ni nini?

Aota ndio mshipa mkuu wa damu (ateri) ambao hubeba damu kutoka kwenye moyo wako hadi sehemu nyingine zote za mwili. Ukuta wa mkole una safu nyingi. Mpasuko mdogo kwenye safu ya ndani husababisha damu kuingia kwenye ukuta wa mkole. Kisha shinikizo la damu hutenganisha safu ya ndani na safu ya kati ya mkole. Utengano huu kunaitwa mgawanyiko.

Mgawanyiko unaweza kuendelea kukua kwenye mkole, iwapo mpasuko kwenye utando utabaki wazi. Hii hutoa nafasi kwa damu kutiririka pale isipopaswa. Mpasuko unavyozidi kukua, unaweza kufunga mishipa midogo ya damu iliyounganishwa na mkole au kuzuia mtiririko mzuri wa damu kwenye mkole.

  • Shinikizo la juu la damu ni sababu ya kawaida ya kupasuka kwa mkole

  • Unaweza kupata maumivu makali ya ghafla kwenye kifua au mgongo wako katikati ya mabega yako

  • Madaktari wanaweza kukupa dawa ya kupunguza shinikizo la damu na kufanya upasuaji wa kurekebisha mpasuko

  • Karibu nusu ya visa vya mgawanyiko wa mkole hutokea kwa watu wa zaidi ya miaka 60

Kuelewa Mgawanyiko wa Mkole

Katika mgawanyiko wa mkole, safu ya ndani (utando) ya ukuta wa mkole huchanika, na damu hupanda kupitia mpasuko, na kutenganisha (kugawanya) safu ya kati na safu ya nje ya ukuta. Kufuatia hayo, njia mpya bandia hutokea kwenye ukuta.

Mgawanyiko wa mkole husababishwa na nini?

Sababu kuu ya kuchanika kwa mkole ni kuwa na shinikizo la juu la damu kwa muda mrefu.

Sababu zisizotokea sana za kuchanika kwa mkole ni pamoja na:

  • Magonjwa ya kijeni katika familia na kuharibu tishu za mwili wako, kama vile Ugonjwa wa Marfan

  • Kasoro za kuzaliwa kwenye moyo na mishipa ya damu

  • Hali ya ateri kuwa ngumu, ambayo inaweza kuzuia mtiririko wa damu kwa viungo na tishu (atherosklerosisi)

  • Majeraha ya kifua, kama vile ajali ya gari au kuanguka

Dalili za kuchanika kwa mkole ni zipi?

Dalili kuu ni maumivu ya ghafla, makali sana. Wakati mwingine maumivu ni makali sana mpaka yakasababisha kuzirai. Mara nyingi maumivu haya hutokea kwenye kifua au mgongo katikati ya mabega yako. Inaweza pia kutokea kwenye sehemu ya tumbo au sehemu ya chini ya mgongo.

Kupasuka kwa mkole kunaweza kusababisha matatizo mengine, kama vile:

  • Kiharusi

  • Shambulio la moyo au matatizo mengine ya moyo

  • Figo kushindwa kufanya kazi

  • Uharibifu wa neva au uti wa mgongo ambao husababisha kutetemeka au kutoweza kusogeza miguu yako

Madaktari wanawezaje kujua kama nina mgawanyiko wa mkole?

Dalili huwa wazi kwa madaktari. Ili kuhakikisha kuwa ni mgawanyiko, madaktari wanaweza kufanya vipimo, kama vile:

Madaktari hutibu vipi mgawanyiko wa mkole?

Madaktari watakulaza hospitalini Utapewa dawa za kupunguza shinikizo la damu na mapigo ya moyo. Shinikizo la juu la damu na mapigo ya moyo ya haraka hufanya mgawanyiko kuzidi kukua kwa haraka. Kisha madaktari wataamua kama watafanya upasuaji.

Upasuaji

Wakati wa upasuaji, madaktari huondoa eneo kubwa la mkole lililochanika kwa kadiri iwezekanavyo. Pia watatengeneza upya mkole kwa mrija (kipandikizi). Ikiwa vali ya mkole inavuja, watairekebisha au kuibadilisha.

Katika migawanyiko isiyo mibaya sana, madaktari wanaweza kuingiza kipandikizi kwenye mkole wako kupitia ateri kwenye mguu wako wa juu ili kurekebisha mpasuko.

Dawa

Iwe umefanyiwa upasuaji au la, utahitaji dawa za kupunguza shinikizo la damu. Dawa zako zinaweza kujumuisha:

  • Vizuizi vya ACE, ambavyo hupanua mishipa yako ili kupunguza shinikizo la damu

  • Vizuizi vya Beta, ambavyo hupunguza kasi ya mapigo yako ya moyo

  • Dawa za kupunguza lehemu, ikiwa mishipa yako ni migumu na iliyosinyaa (atherosklerosisi)