Kuvimba kwa mrija wa mkojo

Imepitiwa/Imerekebishwa Jun 2023

Je, ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo ni nini?

Ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo ni maambukizi ya mrija wako wa mkojo, ambao ni mrija unaounganisha kibofu chako cha mkojo ambao huwezesha mkojo kutiririka nje ya mwili wako.

  • Ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo kwa kawaida husababishwa na bakteria unayopata kutokana na ngono (maambukizi ya zinaa)

  • Dalili za kawaida ni maumivu na kuungua unapokojoa na kuhisi haja ya kukojoa mara nyingi zaidi au kwa nguvu zaidi.

  • Wakati mwingine majimaji hutoka kwenye mrija wako wa mkojo ambayo ni mazito na ya manjano ya kijani kibichi, au yasiyo na rangi na laini

  • Dawa za kuua bakteria kwa kawaida hutibu ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo

  • Ikiwa hutatibu ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo, unaweza kupata maambukizi ya kibofu au ya figo au kidonda kwenye mrija wako wa mkojo

Njia ya Mkojo

Je, ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo husababishwa na nini?

Ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo kwa kawaida husababishwa na:

Je, dalili za ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo ni zipi?

  • Maumivu au kuungua unapokojoa

  • Kuhisi haja ya haraka ya kukojoa mara kwa mara

  • Kwa mgonjwa aliye na kisonono, majimaji mazito, ya manjano-kijani yanatoka kwenye mrija wako wa mkojo

  • Kwa mgonjwa aliye na klamidia, wakati mwingine majimaji yasiyo na rangi na membamba yanayotoka kwenye mrija wako wa mkojo

Ikiwa ugonjwa wako wa kuvimba kwa mrija wa mkojo haitatibiwa, tishu za kovu zinaweza kutokea na zinaweza kufanya mrija wako wa mkojo kuwa mwembamba (hii inaitwa kupungua kwa ukubwa wa mrija). Kupungua huku na kuwa mwembamba kunaweza kufanya iwe vigumu kukojoa. Inaweza pia kuongeza hatari yako ya kupata maambukizi ya kibofu au maambukizi ya figo.

Je, madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo?

Daktari wako anaweza kujua ikiwa una ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo kwa:

  • Vipimo vya mkojo wako au majimaji yanayotoka kwenye mrija wako wa mkojo

Je, madaktari hutibu vipi ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo?

Madaktari hutibu ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo kwa njia tofauti kulingana na chanzo. Kwa kawaida, hutoa dawa za kuua bakteria Ikiwa una maambukizi ya zinaa (STI), mwenzi wako wa ngono atahitaji pia kutibiwa. Hamupaswi kufanya ngono hadi wewe na mwenzi wako mtibiwe kikamilifu.

Je, ninawezaje kuzuia ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo?

Magonjwa ya zinaa ambayo husababisha ugonjwa wa kuvimba kwa mrija wa mkojo yanaweza kuzuiwa kwa kutumia kondomu wakati wa ngono.