Ugonjwa wa baridi yabisi wa kuambukiza ni nini?
Ugonjwa wa baridi yabisi ni uvimbe kwenye kiungo. Kuna aina nyingi za Ugonjwa wa baridi yabisi Ugonjwa wa baridi yabisi wa kuambukiza ni ugonjwa wa baridi yabisi unaosababishwa na maambukizi ya bakteria katika kiungo.
Kiungo chako kinaweza kuambukizwa ikiwa maambukizi mengine katika mwili wako yatasambaa kwenye kiungo, au ikiwa kiungo chako kitapata maambukizi wakati wa upasuaji au kutoka kwenye jeraha
Kwa kawaida kiungo kimoja kikubwa, kama vile goti au bega lako, huathirika
Kiungo chako kitavimba, kuwa chekundu na kuuma, na unaweza kupata homa
Ikiwa kitaachwa bila kutibiwa, ugonjwa wa baridi yabisi wa kuambukiza unaweza kuharibu kiungo chako
Madaktari hutibu maambukizi kwa kutumia dawa za kuua bakteria na wakati mwingine upasuaji ili kutoa usaha kwenye kiungo chako
Je, nini husababisha ugonjwa wa baridi yabisi wa kuambukiza?
Kiungo kinaweza kupata maambukizi kutokana na:
Jeraha la kukatwa, kuumwa au kutobolewa kwenye kiungo
Maambukizi ya ngozi karibu na kiungo
Upasuaji kwenye kiungo
Kisonono ambacho husambaa hadi kwenye viungo vyako
Una uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa baridi yabisi wa kuambukiza ikiwa:
Una kiungo bandia
Unatumia sindano kujidunga dawa za mtaani
Una tatizo la matumizi ya pombe
Una ugonjwa wa baridi yabisi ya rumatoidi, ugonjwa unaoharibu gegedu la maungio ya mifupa, au matatizo mengine ya viungo
Zipi ni dalili za ugonjwa wa baridi yabisi wa kuambukiza?
Kwa kawaida maambukizi ya kiungo huanza kwa haraka. Kiungo chako hupata:
Chungu sana
Wekundu na hali ya uvuguvugu
Huvimba na kuwa kigumu
Wakati mwingine, hupata homa na mzizimo
Kwa watoto wachanga na watoto ambao ni wadogo sana wasioweza kuzungumza, inaweza kuwa ngumu kujua kinachowasumbua, lakini dalili zinaweza kujumuisha:
Kushindwa kusogeza kiungo kilichoambukizwa
Kuudhika
Kukataa kula
Homa
Kukataa kutembea ikiwa kiungo kilichoambukizwa kiko mguuni
Madaktari wanawezaje kujua ikiwa nina ugonjwa wa baridi yabisi wa kuambukiza?
Madaktari watafanya:
Kwa kuchukua sampuli ya majimaji kutoka kwenye kiungo chako kwa kutumia sindano na kufanya vipimo
Ili kufahamu chanzo cha maambukizi ya kiungo chako, madaktari wanaweza kufanya:
Vipimo vya damu
Vipimo vya kiowevu cha uti wa mgongo na mkojo
Eksirei, MRI (upigaji picha kwa mvumo wa sumaku), au upigaji picha kwa mawimbi ya sauti kwa kiungo
Je, madaktari wanatibu vipi ugonjwa wa baridi yabisi wa kuambukiza?
Madaktari hutibu ugonjwa wa baridi yabisi wa kuambukiza kwa kutumia:
Dawa za kuua bakteria au dawa ya kuvu
Kwa kuondoa usaha kwenye kiungo chako kwa kutumia sindano au wakati mwingine kwa njia ya upasuaji
Kuweka kibanzi kwa kiungo, ikifuatiwa na tiba ya viungo
Dawa ya maumivu isiyohitaji agizo la daktari, kama vile aspirini au ibuprofeni